WAZIRI MKUU SOMALIA ATIMULIWA LEO
Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu wa taifa hilo Abdiweli Sheikh
Ahmed mamlakani.
Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa
baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia.
Waandishi wanasema kuwa serikali ilikuwa imelemazwa na uhasama baina ya
kiongozi huyo na rais wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.
Wanasema kuwa usalama ulikuwa umezorotoa kutokana na hali hiyo.
Abdiweli ni waziri mkuu wa pili kuwahi kuondolewa madarakani mwaka huu.
Marekani imeshtumu kura hiyo ikisema kuwa haikuzingatia maslahi ya raia
wa Somali.
No comments:
Post a Comment