PSPF YATOA MSADA WA MADAWATI BUYUNI II - CHANIKA, DAR ES SALAAM
Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko wa Pen sheni wa PSPF, Abdul
Njaidi, (Kushoto), akipena mikono na Ummy Shaaban, mwanafunzi wa darasa
la sita shule ya msingi Buyuni II, iliyoko Chanika, wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam,wakati akikabidhi msada wa madawati kwa ajili ya
shule hiyo mwishoni mwa wiki. (Katikati ni mwalimu mkuu wa shule hiyo,
Rogather Palla.
Mwalimu Mkuu wa shule, Rogather Palla (Kulia), akitoa shukrani
Njaidi, (Kushoto), akitoa elimu kupitia vipeperushi kwa baadhi ya walimu wa shule hiyo
Wanafunzi wakibeba dawati kupeleka darasani
Kikwete na mambo manne hukumu ya Escrow kesho

Katika hukumu ambayo Rais Kikwete ataitoa kesho, suala la maazimio ya Bunge kuhusu kuwawajibisha viongozi waandamizi wa serikali ambao aliwateua, linatarajiwa kupata ufumbuzi.
Hawa ni pamoja na mawaziri, Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini); Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Azimio la Bunge lilitamka wazi kwamba mamlaka ya uteuzi wao ambayo ni Rais Kikwete, atengue nafasi zao kutokana na kuhusika kwao katika kashfa hiyo.
RAIS JK ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JESHI
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza
Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni
maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya
maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini
Arusha jana.
Rais
Kikwete akitunuku Kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha Jeshi huko
Monduli Mkoani Arusha jana. Jumla ya maafisa 171 walitunukiwa kamisheni
wakati wa hafla hiyo. (Picha na Freddy Maro.)
No comments:
Post a Comment