Monday, December 22, 2014

Habari njema kwa Wakenya…waja na teknolojia mpya ya kupima magonjwa ya zinaa kwa njia ya mtandao

lab
Hii ni habari nzuri kwa Wakenya! Imeelezwa kuwa wale wote wanaojihisi kuwa na magonjwa ya zinaa ama kutaka kujua afya zao sasa imepitishwa kuwa kutakua na utaratibu maalum wa kupima na kutoa majibu kwa usiri mkubwa bila mtu yoyote kutambua.
Maamuzi hayo yaliamuliwa na mtaalam Lancet Kenya ambaye alifanya uchunguzi na kugundua  watu wengi wanaogopa kupima kutokana na wataalam  kushindwa kuwatunzia siri zao.
Sasa si muuguzi wala mgonjwa atakayeweza kuonana na mwenzake zaidi ya kutumiwa majibu yake kwa njia ya mtandao ama ujumbe katika simu yake ya mkononi ambapo vipimo vya mgonjwa vitachukuliwa na watu maalum watakaokua wakikaa katika maeneo yatakayopendekezwa na mgonjwa kupeleka vipimo vya damu,mkojo pamoja na maelezo ya jinsi atakavyopewa majibu yake bila kutaja jina.
Kwa sasa Kenya watakua na Uhuru wa kujua afya zao kuhusiana na magonjwa ya zinaa kama Kaswende,Kisonono na hata Virusi vya Ukimwi kwa kukusanya damu kwa njia maalum na ya usiri bila kuweka majina yao na watu wake wa karibu kutojua kinachoendelea.
Baada ya hapo damu hizo zitachukuliwa na kufanyiwa uchunguzi katika maabara na majibu yakitoka,wahusika watajulishwa kwa njia iliyo salama na tulivu kwao kupitia njia ya mtandao.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitt na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza



No comments:

Post a Comment