BREAKING NEWS: Mabaki ya ndege AirAsia yaonekana chini ya bahari
|
WATAALAMU wanaosaka ndege ya AirAsia yenye mruko namba QZ8501 wamesema
wameona mabaki ya ndege hiyo kwa kutumia utaalamu wa kusikia mshindosauti
(sonar) chini ya bahari ya Java.
Hata hivyo taarifa waliyoitoa dakika 40 zilizopita wamesema
kwamba hawana uhakika kama ndege hiyo ipo nzima au ni kipande tu kimeonekana.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa ndugu wa abiria waliokuwapoi katika ndege hiyo
wametaarifiwa kuonekana kwa mabaki hayo.
Awali
jana watafutaji hao waliona sehemu ya mabaki yakielea.
Aidha
maiti kadhaa zilizpatikana jana.
Mabaki
hayo yalipatikana umbali wa kilomita
100-200 kutoka eneo la mwisho ambalo rubani alifanya mawasiliano ya kutaka
kubadili njia.
No comments:
Post a Comment