WEMA KORTINI TENA! KIFUNGO KIPO NJE NJE
Mmoja wa vijana
walioshambuliwa kwa kipigo nyumbani kwa wema.
Mkono wa sheria!
Achana na drama zake na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, mcheza sinema ‘grade one’ Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
anapandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar
kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri,
wakazi wa jijini Dar
HAYUKO PEKE YAKE
Katika kujibu
kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man
naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.
Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana
kufanya kazi na staa
wa huko, Van Vicker, Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu
wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na Juma, tukio
ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama
jijini Dar.chanzo GPL
No comments:
Post a Comment