MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI SAMPULI ZA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA MADARASA YA AWALI KATIKA MANISPAA YA LINDI MJINI
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando
mara baada ya kuwasili kwenye viwanja wa Shule ya Msingi Rahaleo iliyoko
Manispaa ya Lindi Mjini kwa ajili ya kukabidhi sampuli za madawati
aliyoyatoa kupitia taasisi yake kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya
madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Baadhi
ya wanafunzi wanaosoma Madarasa ya Awali katika Shule ya Msingi ya
Rahaleo wakiwa pamoja na walimu wao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya
kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati anawasili shuleni hapo
tarehe 15.12.2014.
Sampuli
za madawati yaliyotolewa na Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali
katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba
fupi kabla ya kukabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi
yake kwenye shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika
Manispaa ya Lindi Mjini kwenye sherehe fupi iliyofanyika kwenye Shule ya
Msingi Rahaleo tarehe 15.12.2014.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za
madawati yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi
Ndugu Gift Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali
katika Manispaa ya Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye
Shule ya Msingi ya Rahaleo tarehe 15.12.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma
darasa la awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama
Salma kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa
ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa Mkoa wa Lindi, wanafunzi wa madarasa ya awali wanaosoma katika Shule
ya Msingi Rahaleo na walimu wao wakati wa sherehe ya kukabidhi sampuli
za madawati tarehe 15.12.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment