Askari Polisi wa wilayani Rungwe wakibeba mwili wa Marehemu Bi Zawadi Mwasongela
Mwili wa Marehemu wakiupakia katika gari ya Polisi kwa ajili ya kuupeleka
hospital ya Wilaya ya Rungwe, Makandana kwa ajili ya kuuthibitisha.
Wanakijiji wa kijiji cha Mwambegele Tukuyu wakishuhudia mwili wa
Marehemu Ukipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe, Makandana.
Namba ya Gari iliyohusika na ajali hiyo.
Mashuhuda wa Ajali hiyo
Ni ajali iliyotokea katika Kijiji cha Mwambegele wilayani Rungwe nje
kidogo ya Mji wa Tukuyu barabara kuu iendayo nchi jirani ya Malawi.
Ajali hiyohiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye usajili namba T372 BYB,
Likitokea nchi jirani ya Malawi kwenda Dar es salaam likiwa na shehena ya mbao zenye thamani ya Tsh 50ml.
Mashuhuda wa ajali wanadai kuwa Gari hilo lilishuka mtelemko kwa kasi
sana inahisiwa kuwa breki za gari hiyo zilifeli na kupelekea Dereva wa
gari hiyo kushindwa kuimudu kona iliyokuwa mbele na kuingia bondeni
ambako kuna mto.
Mto huo hutumika na wakazi wa kijiji hicho kwa bahati mbaya sana Bi
Zawadi Mwasongela alikuwa katika ujenzi wa nyumba yake alienda mtoni
kuteka maji kwa ajili ya ujenzi huo na kukutana na ajali hiyo mbaya
iliyokatisha maisha yake.
marehemu ameacha Mume Watoto 6 na wajukuu 2.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe Amen!!!!
No comments:
Post a Comment