Sunday, December 21, 2014

Real Madrid walivyotwaa ubingwa wa dunia jana Morocco


Klabu ya Real Madrid ya Uhispania jana ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa klabu bingwa ya dunia wakiwarithi FC Bayern Munich.
IMG_0128.PNG
Wakicheza kwenye uwanja wa Marrekech, nchini Morocco Madrid jana walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya San Lorenzo na kufanya idadi ya makombe waliyochukua kufikia matatu – walianza na Copa Del Rey, kisha Champions League na sasa klabu bingwa ya dunia.

IMG_0129.PNG
Sergio Ramos na Gareth Bale walifunga magoli ya ushindi katika mchezo huo.
Kwa ushindi wa jana Real Madrid wameweka rekodi ya kuchukua ubingwa huu wa dunia kwa vilabu kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment