Ni North West… mtoto wa Kim Kardashian alivyojichanganya na watoto wenzake jana
Awali mtoto wa mastaa Kim Kardashian na mumewe Kanye West ilikua ni vigumu kuonekana lakini sasa wazazi wa mtoto huyo wameonekana kumpa mtoto wao uhuru na safari hii mtoto huyo alikua akivinjari na kucheza katika fukwe za Staples center Los Angeles na watoto wenzake ambao ni binamu zake.
Wakati watoto hao wakifurahi pamoja jana
familia hiyo iliongeza furaha baada ya Dada wa Kim Kardashian, Kourtney
na mumewe Scott Disick kujaliwa mtoto wa kiume ambaye anaongeza idadi ya
familia hiyo na kufikisha watoto watatu.
North ambaye kwa sasa amefikisha miezi 17
alipelekwa kwenye fukwe hizo akiogozana na watoto wawili wa dada wa staa
huyo Kourtney ambaye kwa sasa ni mzazi,ambao ni Penelope na mdogo wake
Mason pamoja na watoto wengine wa rafiki wa karibu wa familia hiyo.
North akiwa sambamba na wazazi wake alikua
amevalia koti jeusi pamoja na suruali ya kubana pamoja na viatu aina ya
buti rangi ya brown alionekana kufurahi na watoto wenzake huku wazazi
wao wakiwaangalia kwa ukaribu.
No comments:
Post a Comment