Tuesday, December 23, 2014

Hii ndiyo zawadi ambayo Iggy Azalea ameamua kumzawadia Boyfriend wake kwa ajili ya Krismas

garWakati kilele cha sikukuu ya Krismas ikiwa ni keshokutwa mastaa mbalimbali wameendelea kuonyesha kusherehekea kwa kufanya matukio mbalimbali ikiwa kama ni ishara ya kuhitimisha furaha yao.
Staa huyo ambaye hivi karibuni amejizolea tuzo tatu za American Music Awards 2014 kwa upande wa hipo hop ameamua kumzawadia Boyfriend wake Nick Young gari kama zawadi kwake ya sikukuu ya Krismas.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Iggy kwa sasa ana utajiri wa dola milion 5 na zawadi yake haikua ya bei rahisi kwa sababu ametumia zaidi ya dola 100,000
Nick Young ameonekana kuifurahia zawadi hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo alimshukuru kwa zawadi hiyo ya krismas na kusisitiza anampenda sana.

No comments:

Post a Comment