U Heard ya leo December 22 iko hapa, inamhusu msanii Ney wa Mitego.
U Heard ya leo December 22 inamhusu msanii Ney wa Mitego ambapo
story ni kwamba kuna taarifa za msanii huyo kwenda Kenya kwa ajili ya
kufanya video ya wimbo wake mpya lakini kutokana na ratiba ya Director
aliyehusika kushoot video hiyo kugonganisha ratiba ya Ney na Wizkid, ikabidi Ney
asubiri kazi hiyo iishe ndipo ya kwake ianze ambapo ilifanyika chini ya
kiwango hivyo Ney akaamua kuirudia video hiyo Dar na Director mwingine
kutoka Kenya.
Ney amesema amefanya maamuzi ya kuirudia
video yake kwa sababu Dar pia ina mazingira yote mazuri ya kufanyia
video, hivyo akaamua kuirudia video hiyo na kwa sasa hayuko tayari
kuzungumzia kuhusu kilichotokea.
Ney
amesema kuwa video zote mbili zimemgharimu zaidi ya milioni 36, lakini
kama ile moja angeridhishwa nayo gharama zake zisingefikia kiwango
hicho.
No comments:
Post a Comment