THE MBONI SHOW YAANZA KUUNGURUMA JANUARY 2 NDANI YA TBC
Mkurugenzi wa
Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi
wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es
Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The
Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti Simpompa
na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili
Chilumba.
Kutoka Kulia
Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema
akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika
Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa
Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa
Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show
katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia
watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano
wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi
cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna
atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa
vile ana hati miliki.
“Nimeamia TBC
kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna
atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya
jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande
wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema
wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa
wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na
wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini
wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema
wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha
pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.
No comments:
Post a Comment