Janga la ajali ya boti mtoni, miili yapatikana wengine haijulikani walipo
Usafiri wa majini umekuwa usafiri mkubwa unaotegemewa katika maeneo
ambayo yamekuwa na changamoto ya miundombinu katika nchi ya Congo.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari Congo Lambert Mende,
amethibitisha kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya watu 129
iliyotokana na boti ya MV Mutambala kujaza watu kupita kiasi ambapo
ilikuwa na watu zaidi ya 300 na kusafiri wakati wa usiku kitu ambacho
hakiruhusiwi.
Boti hiyo ilizama mto Kasai umbali wa kilometa 50 kutoka Mji wa Tshikapa.
No comments:
Post a Comment