MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI TAMASHA LA UPENDO WA MAMA DAR
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa
kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika
katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na
kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya
Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia
Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha
hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua
mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.
Injinia
Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya
uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha
waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado
Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam.
Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.
Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye
atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao
watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya
Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na
waimbaji wengine wengi.
"...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na
zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati
itakapotangazwa...kutakuwa
na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta
mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango
wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi.
Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na
litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni
litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi
maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika
familia zao.
Rais
wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa
lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo
juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.
Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa
matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza
tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.
No comments:
Post a Comment