Story ya mwanamke anayelaza waume za watu kwenye Pub yake, #Hekaheka ya December 30
Wanawake wawili wamelalamikia kitendo
cha dada mmoja ambaye amefungua pub ya kuuza vinywaji, lakini wanawake
hao wamesema kuwa mwanamke huyo ameweka magodoro mawili ambapo
ametuhumiwa kuwa anawalaza wanaume za watu ndani ya Pub hiyo.
Mwanamke mmoja amesema kuwa waliuza
nyumba na mumewe na wakaamua kujenga nyumba nyingine lakini mwanaume
huyo alimtelekeza mkewe eneo la ujenzi na kwenda kunywa pombe katika Pub
hiyo, alipomfuata mwanaume huo aligoma kuondoka hivyo mwanamke akaamua
kumwaga vinywaji vilivyokuwa kwenye meza na kupelekea ugomvi kati yao.
Wanawake hao waliandamana kwenda kwenye
Pub ya mwanamke huyo ili wakamseme kuhusu tabia hiyo, lakini mwanamke
huyo alikataa kuwa huwa anawalaza wanaume hao katika Pub yake, ila
magodoro ambayo yapo huwa wanayatumia wafanyakazi wake kulala wakati wa
usiku.
No comments:
Post a Comment