Amwacha mumewe na dadake uchi barabarani
Mwanamke kwa jina Ting Su nchini Uchina alimwacha mumewe na dadake bila
nguo barabarani baada ya kuwapata wakifanya mapenzi Ting Ting Su
aligundua kwamba mumewe alikuwa akimdanganya na dadaake na kuwafuata
hadi katika kituo kimocha cha maduka akitumia teknologia katika simu
yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.
Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili
kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikendelea lakini waliwachwa na mshangao
mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka
na kuwawacha wawili hao barabarani bila nguo.
Kulingana na gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema
walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na
yeye hakubakia nyuma.
Mumuwe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.
No comments:
Post a Comment