UNIC YAELIMISHA SIKU YA CHOO KWA VIJANA WALIO NJE YA SHULE
Siku ya choo duniani ambayo huadhimishwa
tarehe 19 Novemba. UNIC waliadhimisha siku hii kwa kuwakutanisha vijana
walioko nje ya shule tarehe 23 Desemba 2014 kwa lengo la kuwaelimisha
na kuwahamasisha utumiaji wa vyoo ili na wao waweze kuelimisha jamii
zinazowazunguka juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo.
Tukio hili liliwakutanisha vijana toka
vikundi 5: Azimio Youth Group, Makangarawe Youth Development Fund,
Mashine Ya Maji Youth Development Centre,Temneke Youth Development
Foundation na Tanzania Youth Development Society. Yafuatayo ni baadhi ya
matukio katika picha.

Vijana wakiwa katika makundi kujadili na kuweka mikakati watakavyosaidia jamii kuhusu utumiaji wa vyoo na usafi wa mazingira.
Afisa Habari wa kituo cha habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma-Ledama akitoa mada kuhusu siku
ya Choo duniani pamoja na umuhimu wa utumiaji vyoo, na kampeni maalumu
ya uhamasishaji wa kuwa na vyoo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za
Vijana Temeke (Temeke Youth Development Network -TEYODEN), Ismail
Mnikite akitambulisha vijana waliohudhuria kutoka makundi mbalimbali.
Baada ya majadiliano, vijana
wakiwasilisha maazimio na mikakati waliyoyakusudia kufanya ndani ya
vikundi vyao katika jamii zinazowaunguka.
No comments:
Post a Comment