Ray: Nikiwa nao wananisifia, nikiwapa kisogo wananisema
Vincent Kigosi ‘Ray’
Ray alisema kuwa baadhi ya wasanii wachanga leo hii
wanauza kazi zao na kukaa na wakongwe na kuwasifia lakini wakiwapa
kisogo wanawasema vibaya.
VINCENT Kigosi ‘Ray’ amesema kuna baadhi ya watu
wakiwamo wasanii, huwa wanawadharau wakongwe walioifanya tasnia hiyo
kuwa juu na kuwasema vibaya pindi wanapowapa kisogo.
Ray alisema kuwa baadhi ya wasanii wachanga leo
hii wanauza kazi zao na kukaa na wakongwe na kuwasifia lakini wakiwapa
kisogo wanawasema vibaya.
“Tasnia hii watu waliisusa ilikuwa ikionekana kama
ni kazi ya ziada tu wala si kazi inayomwezesha mtu kuendesha maisha
yake, katika hali ngumu tulipigana na kuifikisha hapa, wasanii wakongwe
ndio tuliopigania, leo wanatubeza kwa sababu wanauza filamu zao,”
alisema Ray.
Ray alisema hivi sasa tasnia inatolewa macho na
kila mtu kuwa ni ajira kwa watu hata serikali imeliona hilo. Ray alisema
ili kuhakikisha kazi zake zinakuwa bora kila mara hutumia muda mwingi
kuongeza vifaa vya kisasa sambamba na kutumia watu wenye ujuzi wa
filamu.
“Lakini bado najua kuna watu ambao nikiwa nao hujifanya kunisifia nikiwapa kisogo tu huniponda,” alisisitiza.
Ray anashauri vijana washindane katika kazi na si kupoteza muda kwa kuwabeza watu na kuzungumzia majungu.
No comments:
Post a Comment