Balozi Seif Atembelea Jengo la Maabara Kuu Mombasa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na mwenyeji wake
Mrajisi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Dr. Burhan Othman Simai
akikagua Maabara ya Bodi hiyo iliyopo kwenye jengo lao jipya liliopo
Mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mrajisi
wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Dr. Burhan Othman Simai akimpatia
maelezo Balozi Seif juu ya juhudi wanazochukuwa watendaji wa Bodi hiyo
kukagua bidhaa mbali mbali zinazoingizwa nchini ili kujua ubora wake.
Mratibu
wa mradi wa EAC – MRH ulio chini ya Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar
Bibi Hidaya Juma akitoa maelezo ya maendeleo ya mrtadi huo mbele ya
Balozi Seif aliyefika katika Jengo la Bodi hiyo kulikagua.Kushoto ni Mrajisi wa Bodi ya Chalkula na Dawa Dr. Burhan Othman Simai.
Meneja
wa Kitengo chaMtandao wa mawasiliano ya Kompyuta cha Bodi ya Chakula na
Dawa { ZFDB } Ndugu Mohamed Yahya Said aliyevaa shati rangi ya buluu
akielezea mfumo wa Mradi wa MRH unaotoa fursa kwa Bodi ya Chakula na
Dawa kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja ya mamlaka za Bodi nyengine
Duniani.(Picha na Hassan Issa OMPR)
No comments:
Post a Comment