Wednesday, December 24, 2014

TANGAZO…………… TANGAZO…………………………TANGAZO.


KAMPUNI YA SMART COMMUNICATION GENERAL ENTERPRISE LTD (SCGE) inapenda kukukaribisha katika usiku wa kihistoria wa zawadi maalum kwa wanandoa utakaoweka historia mpya tangu kuanza kwa ndoa yako.
Siku hii maaluma ya kukumbukwa itakuwa tarehe 26/12/2014 yaani siku ya Chrismas Box ambayo watu wote duniani huitumia kwa ajili ya kupeana zawadi, Lakini wewe siku hiyo utaitumia kwa ajili ya kupeana zawadi kwa mwandani wako ndani ya Ukumbi wa Mkapa kuanzia saa 12 jioni.
Siku hii itapambwa na burudani kabambe za muziki wa aina mbali mbali utakaowafanya mjisikie kutojutia kuwa ndani ya ndoa, pia kutakuwa na mafundisho kwa Walimu wa NDOA waliobobea ambao watakueleza nini maana ya ndoa, faida zake, furaha ya ndoa, siri ya ndoa inayodumu miaka mingi  na mengine mengi.
Pia kutakuwa na chakula kizuri na vinywaji, njoo na mwenzi wako ambapo viongozi mbali mbali na watu maarufu wakakuwepo wakiwemo viongozi wa serikali katika Mkoa wa Mbeya.
Ili kufanikisha maandalizi na usiku huu wa ajabu kwako unaombwa kuchangia shilingi elfu hamsini(50,000/= tu )
Mungu akubariki na ahsante kwa utayari wako, njoo tufurahi pamoja na kujua  mpango wa Mungu kwa wanandoa.
Kwa mawasiliano zaidi;
Charles Mwakipesile (Mratibu mkuu) 0754- 301848
Au Mtumuli 0755- 367723.

No comments:

Post a Comment