WAZIRI GHASIA ATOA KAULI KUHUSU DOSARI ZA UCHAGUZI WA JANA
Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia akizungumza na Waandishi wa Habari leo Picha na Suleiman Magari |
Na Karoli Vinsent
SERIKALI
nchini imekili Uchaguzi uliomalizika jana wa Serikali za Mitaa
ulikuwa na Dosari katika baadhi ya Maeneo mbalimbali nchini na kusema
itawachukulia Hatua kali za Watendaji Halmashauri Mbalimbali
waliopelekea kuwepo na Dosari hizo.
Pia Licha ya kuwa na Dosari lakini Bado Serikali imesema uchaguzi huo umefanikiwa kwa asilimia 98,Tofautisha na Miaka mingine.
Hayo yemesemwa leo Jijini Dar Es Salaam naWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa
Gasia wakati wa Mkutano na Waandishi ili kuzungumzia uchaguzi huo wa
Serikali za Mitaa ambapo pamoja na Mambo Mengine Waziri Gasia alikili
kuwepo na Dosari kwenye Vituo mbalimbali vya kupiga kura katika baadhi
ya Kata,Vijiji,Mtaa au Vitongoji
Waziri
Gasia alizitaja Dosari hizo ambazo ni kukosekana na Ujio wa Vifaa vya
Kupigia Kura,Kasoro za karatasi za kupigia kura,wapiga kura majina yao
kutokuwepo katika vituo pamoja na kuwepo na udangachifu kutoka kwa
wapiga kura.
Pichani ni Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari Tofauti wakimsikiliza kwa makini Waziri Hawa Gasia |
Vilevele
Waziri Gasia alisema Halmashauri na Maeneo yenye Kasoro ambayo
hayakufanya Uchaguzi,yatarudia uchaguzi huo ndani ya Siku (7) kama
kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinavyoelekeza.
Aidha,Waziri
Gasia aliitaja Mikoa ambayo Dosari zilijitokeza na kupelekea
kuhailishwa kwa uchaguzi huo katika baadhi ya Kata, vitongoji na Vijiji
ni, Kilimanjaro ,
Manyara,Morogoro,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Dar
Es Salaam,pmoja na Mkoa wa Pwani.
Waziri
Gasia aliongeza kuwa kwa ujumla Halmashauri ambazo hazinadosari ni 145
kati 162 zilizofanya uchaguzi ambapo Halmashauri tatu kati ya hizo
hazikufanya Uchaguzi kabisa kutokana na kucheleweshwa kwa Vifaa.
Hatahivyo
Waziri Gasia aliziagiza Halmashauri hizo uchaguzi kufanya haraka ndani
ya siku 7 na vilevile Wizara hiyo ya TAMISEMI itawachukuli hatua kali za
watendaji waliopelekea Dosari hizo.
“Tumeitaka
Mikoa Iwasilishe Taarifa rasmi na kamiilifu kuhusu Kilichojitokeza
katika Halmashauri hizo na Wizara itachambua taarifa hizo ili kubaini
wote waliosababisha kasoro wachukuliwe hatua stahiki ikiwemo kusimamisha
kazi,kukatwa mishahara,pamoja na kufukuzwa kazi”alisema Waziri Gasia.
Waziri Gasia aliongeza kuwa licha ya uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali
za Mitaa kuwepo na Changamoto mbalimbali lakini serikali imefanikiwa
uchaguzi huu kwa asilimia 98 tofautisha na miaka mingine.
No comments:
Post a Comment