Friday, April 10, 2015

Zijue faida 11 za kulala uchi au mtupu nyakati za Usiku




UMEZOEA kulala na nguo nyepesi za kulalia? Au unahisi vizuri zaidi ukilala na nguo nzito laini za kulalia? Watu wengi hujifunika mashuka na wengine hujifunika mablenketi kabisa.


Katika makala haya, FikraPevu itakufumbua macho uanze kulala uchi/mtupu kwa kutumia hoja bora zilizochaguliwa kuelezea kwanini kulala uchi ni kuzuri kwako.


Nguo za kulalia zina gharama kubwa
Ni kiasi gani cha fedha ambazo wewe hutumia kununua pea ya nguo za kulalia? Inaweza kuwa kati ya fedha za kitanzania kati ya shilingi 20,000 na 40,000 au zaidi. Ni mara ngapi huzifua hizo nguo? Sasa fikiria ni kiasi gani cha pesa na muda unachoweza kuokoa usipovaa nguo za kulalia.


Hutengeneza uhusiano mzuri ukisaidiwa na kichocheo cha Oxytocin
Natasha Turner, daktari wa tiba asilia aliyeandika kwenye blogu ya Huff Post Canada, alifichua kwamba kulala karibu au mkiwa mmekumbatiana na mwenzi wako mkiwa uchi/watupu hufanya mwili kutoa kichocheo kiitwacho Oxytocin kinachofanya ujisikie vizuri. Hii inatokea pale kunapokuwa na mgusano wa ngozi kwa ngozi, hii inaweza kusaidia kuondoa msongo (Stress) na kushuka moyo (Depression).


Oxytocin pia inaweza kupunguza shinikizo la damu, kuimarisha tumbo na kupunguza uvimbe kwenye utumbo. Pia, utendaji wako wa tendo la ndoa pengine unaweza kuboreka.


Hupelekea usingizi mwanana
Hivi unafahamu baadhi ya matatizo ya kukosa usingizi (Insomnia) yanaambatana kutokana na tatizo la mwili kudhibiti jotoridi? Taasisi ya Usingizi ya Los Angeles inaripoti kwamba hali hii haiathiri tu mzunguko wa usingizi ila pia hukuzuia kupata usingizi mnono. Kulala uchi/mtupu husaidia katika kurekebisha jotoridi la mwili (hivyo mwili hauchemki kupita kiasi, ni vibaya kuamka umelowana jasho.

Hukufanya ubaki kijana
Kama tulivyoona hapo juu kuhusu kudhibiti jotoridi kama unahitaji usingizi mzuri, Natasha Turner anashauri kuweka mwili katika jotoridi chini ya 21°C ukiwa kitandani na njia nzuri kufanta hivyo ni kulala uchi/mtupu. Hii huruhusu vichocheo vinavyozuia uzee na Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa kusinzia na kuamka kutenda kazi vizuri.

Utajihisi huru, Kulala kitandani kwako, bila kuvaa chochote inakufanya kujisikia huru.

Huhamasisha vichocheo vya furaha (kuponya)
Unapolala na nguo au kulala chini ya blanketi zito unazuia utokaji wa kichocheo cha ukuaji (Growth Hormone/HGH). Hii ina maana hutoweza kupunguza mafuta ukiwa katika usingizi au hautofaidika na ukarabati wa usiku wa mifupa, ngozi na nyama za mwili wako.

Kulala uchi/mtupu pia huthibiti kiwango cha Cortisol, zinazo dhoofisha kinga ya mwili, kupandisha shinikizo la damu na lehemu (Cholestrol), kuvuruga mpangilio wa usingizi, kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuongeza hamu ya sukari.

Inaimarisha kujipenda
Kama una matatizo ya kutokujiamini basi kulala uchi/mtupu kutakusaidia kujifunza kujipenda. Kwa kuanza, jizoeshe kulala bila nguo kila jioni. Baada ya muda utazoea pia baada ya muda unaweza kuwa umejifunza kuupenda muonekano wako bila nguo.
Inatunza kiafya viungo vya uzazi.
Kina dada, mnafahamu mnaweza kupunguza matatizo ya mabukizi ya fangasi kwa kulala uchi/watupu? Unaweza kupunguza kuzaliana kwa fangasi na uke wako utakushukuru kwa hilo. Vilevile wanaume wanaweza kufaidika kulala uchi/watupu kwa kuwa korodani zinakuwa katika jotoridi la kutosha na uzazi unaongezeka.

Mzunguko wa damu unakuwa bora
Hakuna kitu kibaya kama lastiki inayozuia mzunguko wa damu. Ondoa nguo zenye lastiki na utajipata uko na furaha kwa mtiririko wa damu mzuri ndani mwili wako.

Kuwa na ngozi nzuri
Unapokuwa uchi/mtupu ngozi yako inapata nafasi ya kupumua. Kama una chunusi au vipele mgongoni ni kitu cha thamani kuacha hewa ya Oxygen kufika kwenye maeneo hayo. Ngozi yako inastahili uhuru kidogo na utajisikia vizuri kwa kuiacha ngozi wazi.
Kutokuwa mvivu
Faida nyingine ya kulala uchi/mtupu ni kwamba mara baada ya kuamka unakuwa na ulazima wa kuvaa nguo kwa ajili ya siku hiyo mpya na sio kuamka na nguo zako za kulalia na kutoka nazo nje.

Jumatatu, 6 Aprili 2015

Polisi Ajiua Kwa Kujipiga Risasi.




Askari wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, H 3416 PC Charles, amejiua kwa kujipiga risasi.

Baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na kituo hicho cha polisi, Paulo Lazaro na Furahisha Felix, walisema tukio hilo lilitokea Aprili 4, mwaka huu, saa 1:00 usiku kituoni hapo.

“Suala hili limetushangaza, kwani sisi tulikuwa nyumbani. Ghafla tulisikia mlio wa bunduki katika kituo cha polisi. Tulipofika, tulimkuta askari huyo akiwa amekufa kwa kujipiga risasi,” alisema Lazaro.

Wananchi hao walisema kutokana na hali hiyo, walilazimika kuwauliza baadhi ya askari waliokuwa zamu, ambao walidai hata wao hawajui ni kwanini mwenzao amechukua uamuzi wa kujiua.

Waliomba ufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kujiua kwa askari huyo kwani inawezekana kuna kitu ambacho alikuwa amechukizwa nacho.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kujiua kwa askari huyo. “Ni kweli askari huyo amejiua kwa kujipiga risasi wakati akiwa kituoni majira ya saa 1:00 usiku,” alisema Kamanda Kaganda.

Hata hivyo, Kamanda Kaganda alisema hakuna ujumbe wowote ulioachwa na askari huyo kuelezea sababu za kujiua. Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kaganda aliwataka askari wote kutatua matatizo yao kupitia kwa viongozi wao badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha askari huyo kujiua.

Alhamisi, 2 Aprili 2015

Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa

**********  

Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho

Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa


Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata


Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao                                                                                                                                                                     ................................................................................                                                                                                               Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
 
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
 
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. 
 
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano  na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
 
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa zaidi ya wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.

Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.

Mwanamke Afanyiwa Ukatili Wa Kutisha Na Mume Wake.....Achomwa Moto Kwa Petrol, Mtoto Wa Mwezi Mmoja Afariki Dunia



Machi 31 mwaka huu, mwanamke mmoja mkazi wa Bwai wilayani Butiama, Kudra Nanja alifanyiwa ukatili na mumewe wa kuchomewa ndani ya nyumba kwa petroli, tukio lililosababisha mtoto wake Tatu Simioni aliyekuwa na umri wa mwezi mmoja u nusu kufariki dunia.

Jumanne, 31 Machi 2015

Mama Awafungia Ndani Watoto Wake Watatu Kwa Miaka 10


Ni mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi  katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.

Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa watu waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.
 
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
 
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
 
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
 
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.
 
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
 
"Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? 
 
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”

Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.

Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
 
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
 
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.
Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
 
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:
 
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
 
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu."
 

Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume  na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).

Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
 
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
 
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
 
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia.
 
 “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
 
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
 
Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

No comments:

Post a Comment