Wednesday, December 10, 2014

KENYA: MASENETA WA CORD WAPINGA MSWADA WA KUKABILI MAGAIDI

Na CHARLES WASONGA
MASENETA wa muungano wa Cord wamepinga Mswada unaolenga kubadilisha sheria za sekta ya usalama nchini wakisema unahujumu haki za kikatiba za raia.
Bw Moses Wetangula. Picha/MAKTABA
Waziri Wetangula
Wakiongozwa na Bw Moses Wetang’ula (Bungoma) viongozi hao walitaja Mswada huo uliowasilishwa na serikali bungeni Jumanne kuwa dhalimu na wakatisha kupeleka kesi kortini kupinga sheria hiyo iwapo Rais Uhuru Kenyatta ataiidhinisha.
“Sisi kama viongozi hatuwezi kukubali Mswada kama huu ambao kimsingi unaondoa haki za kibinadamu ambazo Wakenya walilipigania kwa zaidi ya miongo miwili wakitetea Katiba hii ya sasa ambayo inalinda haki hizo. Kisingizio kwamba hatua hiyo itasaidia vita dhidi ya ugaidi si kweli. Watu wasio na hatia ndio wataumia zaidi,” Bw Wetang’ula akaambia wanahabari kwenye majengo ya Bunge Jumatano.
Alisema kuzorota kwa usalama nchini kunasababishwa na uzembe wa vikosi vya usalama na ufisadi wala sio kasoro katika sheria za usalama.
Maseneta wengine waliokuwa wameandamana naye ni Amos Wako (Busia, ODM), Bonny Khalwale (Kakamega, UDF), James Orengo (Siaya), Johnstone Muthama (Machakos, Wiper) na Mutula Kilonzo Junior (Makueni, Wiper).
“Mashambulizi ya Mandera na yale ya Mpeketoni yalitokana na uzembe wa vikosi vya usalama. Ni wazi pia kwamba baadhi ya maafisa wa polisi hupokea hongo kutoka kwa wahalifu, hasa magaidi, na hivyo kuwaruhusu kupata nafasi ya kuwadhuru Wakenya,” akasema Bw Wetang’ula akitetea pendekezo la magavana la kugatuliwa kwa sekta ya usalama.

Akiwasilisha Mswada huo, kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale alisema una vipengee vinavyofanikisha juhudi za serikali za kupambana na ugaidi, ambao umekuwa kero kubwa la usalama nchini.
Bw Duale alikuwa akizungumza kuhusu msururu wa mashambulizi ya kigaidi ambayo yamesababisha ya Wakenya zaidi ya 64 katika Kaunti ya Mandera na mafunzo ya itikadi za kigaidi kwenye misikiti eneo la Pwani.
Deni
Bw Orengo alisema Mswada huo pia utahujumu uhuru wa wanahabari kutokana na kipengee kinachotoa adhabu kali dhidi ya uchapishaji na usambazaji wa habari na picha zitakazofasiriwa kuwa za kueneza chuki na woga kwa umma.
Wakati huo huo, maseneta hao walipinga hoja iliyopitishwa bungeni Jumanne ambayo itaruhusu serikali kuongeza kiwango cha mkopo wa kigeni kutoka Sh1.2 trilioni hadi Sh2.5 trilioni.
Wanataka hoja hiyo iwasilishwe katika Seneti ili ujadiliwe kwa kina wakisema hatua hiyo inahusu kaunti.
“Mzigo huu wa madeni utaathiri vibaya kiwango cha fedha zinazotengewa serikali za kaunti. Isitoshe, pesa za kulipia madeni ya kigeni zitatokana na ushuru wa Wakenya wote. Hii ndio maana suala hili linafaa kuwasilishwa kwa Seneti,” akasema Bw

No comments:

Post a Comment