Hii ni Good News kuhusu usafiri wa anga Tanzania…

Watu wengi wamekuwa watumiaji wa usafiri
wa anga Tanzania kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni ukilinganisha
na miaka ya nyuma ilivyokuwa, lakini good news ya leo imeripotiwa na
kituo cha ITV ambapo idadi ya mashirika ya ndege kutoka nchi mbalimbali imeongezeka na kufikia 18.
Kuongezeka kwa mashirika hayo kunafanya
kukua kwa huduma hiyo na kurahisisha huduma hiyo kwa wasafiri, lakini
hata Serikali pia inapata pato linalotokana na malipo ambayo kila ndege
inayotua inalipia tozo ambapo malipo hayo huzingatia uzito wa Ndege.
“… Tunafanya kazi na mashirika haya
tunazungumza nao, tumeajiri Consultant ambaye ndio kazi zake hizi routs,
tumekaa naye yeye ndio anazionyesha hizi Airline kwamba ukienda Dar es
Salaam utapata abiria hawa na hawa… siyo inakuwa mtu anakaa tu nyumbani
anaota ndege zinakuja… kazi inafanyika chini ya Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege…”
Hii ni taarifa niliyoirekodi kutoka kituo cha ITV.
No comments:
Post a Comment