WATU WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI, WAMEUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI
Watu
wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi
wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya
shilingi milioni 100 katika kiwanda cha kutengeneza chokaa cha Nelkanth
kilichopo eneo la Amboni jijini Tanga kushindikana.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi wa polisi Juma Ndaki
amewataja majambazi waliouawa kuwa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni
jijini Dar es Salaam na Mwinyimkuu Hamisi mkazi wa mtaa wa Chanika ambao
walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya boxer huku wenzao wawili
wakikimbia kusikojulikana.
Wakielezea
vyema tukio hilo baadhi ya wafanyakazi na walinzi wa kiwanda hicho
wamesema majambazi hao baada ya kuingia ndani ya geti la kiwanda hicho
walikwenda moja kwa moja katika chumba cha mhasibu na walipofika
walianza kunyonga mhasibu lakini wakati wa kujitetea ndipo sekretari wa
mhasibu alipotoka nje ya ofii na kupiga mayoe kuashiria bosi wake
amevamiwa na majambazi.
Kufuatia
hatua hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho Bwana Amiry
Ramadhani ameliomba jeshi la polisi mkoani Tanga kuhakikisha wanafanya
upepelezi wa kutosha ili kujua kama huenda kuna baadhi ya wafanyakazi
ambao wamekuwa chanzo cha tukio hilo.
CHANZO: ITV TANZANIA
CHANZO: ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment