ONA KILICHOWAPATA HAWA MAFUNDI BAADA YA KUIBA NYUMBANI KWA WEMA

Nyumbani kwa muigizaji wa filamu, Wema Sepetu,
kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi,
kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.
Kwamujibu wa Bongo5.com ambao walizungumza jana na
jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo
lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.
“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi
ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama
huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka
wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”
“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika
wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea
huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia
mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili
wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa! Ndo
yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza
kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia
sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo
wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo. Wema ana
roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani
kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana
watamfanyika tukio la kinyama sana,” ameongeza mama huyo.
“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti
likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa
hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya
kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti
wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo
wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya
mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,” alisema Mama
Steve.
Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama
Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. “Hii ni tabia
yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga
makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini
kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,”
alisema.
Kwamujibu wa Bongo5.com,mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana
kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini hakupatikana ilikuthibitisha na kutujuza kile kinachoendelea katika sakata hili.
Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika
kwenye tukio hilo, aliiambia Bongo5.com kuwa watu hao walipigwa lakini
hawakuvuliwa nguo. “Yeah kuna tukio limetokwa,lakini hakuna mtu
aliyevuliwa nguo,” alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.
No comments:
Post a Comment