DIAMOND AMWIMBIA SHABIKI WAKE WIMBO WA SIKU YA KUZALIWA
Diamond Platnumz akimwimbia shabiki wake Osama Mwita kutoka Tanzania
wimbo wa siku ya kuzaliwa siku ya Jumamosi Desemba 6, 2014 kwenye
sherehe ya Uhuru ilizofanyika katika hotel ya Sheraton Downtown Silver
Spring, Maryland nchini Marekani.
Diamond akiendelea kumwimbia shabiki wake huyo ambaye usiku wa Desemba 6, 2014 ilikua ni siku yake ya kuzaliwa.
MKUTANO WA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya
Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati
Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi
wa Chama cha Mapinduzi CCM alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya
CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi
Seif Ali Iddi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai (kulia) wakiwa katika kikao cha siku moja cha Mkutano wa Kamati
Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika leo katika
ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
(NEC) wakiwa katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
ulipofanyika mkutano huo leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Wajumbe wa Sekretarieti wa Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya
CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakiwa tayari kuweka kumbu kumbu kwa mabo
yote yatakayozungumzwa katika Mkutano huo uliofanyika leo chini ya
Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa taarifa kwa
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya
(NEC) katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kiako
hicho kilifanyika leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi (kushoto). Picha
na Ikulu.
MAHAFALI YA 5 YA CHUO KIKUU KIKUU CHA ST, JOHN DODOMA YAFANA.

Mkuu wa chuo kikuu kikuu cha St, John Askofu Dolnad Mtetemela katikati akiwa na viongozi wa kanisa la anglikan ambalo ndilo mmiliki wa chuo hicho walipokuwa kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Philip Alfred aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya tano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St, John's cha mjini Dodoma akihuwahutubia wahitimu wa kozi mbalimbali wa chuo hicho.

Mkuu wa Skuli za kidini akihutubia jambo kwenye mahafali hayo.

Wahitimu wa Shahada ya sayansi katika uuguzi wakila kiapo cha utumishi uliotukuka wakati wa mahafali ya tano ya chuo kikuu cha St, John's kinachomilikiwa na kanisa la anglican kilichopo mjini Dodoma

Meneja wa CRDB Tawi la Dodoma Bi Rehema Hamisi akiwa na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kukabidhi kwa viongozi wa chuo kikuu cha st, John's kama mchango wa maendeleo ya chuo hicho
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Rais Kikwete afanya Kisomo Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kupona
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya Mashekhe na
wageni waliohudhuria hafla ya kisomo maalum cha Kumshukuru Mwenyezi
Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama
kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo
Jumapili Desemba 7, 2014.
Mjukuu wa Rais, Ayman Ridhiwani Kikwete akicheza kwa furaha wakati
Babu yake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wageni na Mashekhe
waliohudhuria hafla ya kisomo maalum kilichofanyika katika viwanja vya
ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumapili Desemba 7, 2014

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mjukuu wake Ayman
Ridhiwani Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya
kumalizika kisomo cha shukran kwa Mwenyezi Mungu kiklichofanyika ikulu
jijini Dar es Salaam leo Jumapili Desemba 7, 2014.(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment