Wednesday, December 3, 2014


COLETHA Raymond (PICHANI) mwigizaji wa kike Bongo amefunguka kwa kusema kuwa tasnia ya filamu imetawaliwa na uchawi kitu ambacho ni vigumu sana kuwaona baadhi ya wasanii kung’ara katika kazi za sinema kwa sababu uchawi hauna ushahidi si rahisi kutamka hadharani.
“Wengi wanaogopa kusutwa lakini lisemwalo lipo na kama halipo laja, suala la uchawi katika tasnia ya filamu lipo wala watu wasikatae unakuta msanii anajua kuigiza lakini kila sinema kapewa scene kidogo au hata akipewa nafasi kubwa haonekani kafichwa,”anasema Coletha.
Msanii huyo anataja baadhi ya wasanii ambao hadi leo wana uwezo mkubwa katika kuigiza lakini hawaonekani hata ukikutana nao hawana hamu ya kuigiza tena kwani pamoja na uwezo wao wa juu hawapewi nafasi wanaopewa nafasi ni wale waliojiweka sawa, anawashauri waingiapo humo wajipange.

No comments:

Post a Comment