Taarifa nyingine kutoka Ikulu kuhusu Rais Kikwete leo Desemba 07
Tulisikia
kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji Marekani, Rais Kikwete alipewa
masharti kadhaa na madaktari waliomfanyia upasuaji juu ya utaratibu wa
kufanya katika kipindi cha miezi mitatu, ambapo moja ya masharti
aliyopewa ni kutofanya kazi ngumu.
Katika ukurasa wa Facebook wa gazeti la Mwananchi, wamepost picha na story inayosomeka hivi; “..MAZOEZI:
Rais Jakaya Kikwete akifanya mazoezi katika Viwanja vya Ikulu, Dar es
Salaam, kutekeleza ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara
tatu kwa siku ili kuimarisha afya yake, baada ya upasuaji mwezi uliopita
nchini Marekani. Picha na Ikulu..“

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Facebook
No comments:
Post a Comment