MSANII JB BONGE LA BWANA KUFUNGA MWAKA NA ‘MZEE WA SWAGA’..MCHEKI HAPA
Ni staa asiyeonekana zaidi katika filamu anazoziandaa akisema anajaribu kupanua wigo wa waigizaji nchini
Dar es Salaam. Anaigiza,
anawaachia nafasi wengine akiwa nyuma ya kamera, anachekesha anapotakiwa
kufanya hivyo, ni mnene wa mwili lakini mwongozaji wa filamu akimwamuru
kukimbia hana budi kufanya hivyo.
Huyu si mwingine ni Jackob Steven maarufu JB, mmiliki wa kampuni ya utayarishaji filamu iitwayo Jerusalem.
Mwanzoni mwa mwaka huu, aliahidi kutayarisha kazi
ya kufungia mwaka ambayo ingetayarishwa katika mikoa kadhaa nchini na
kwa bahati, amelikamilisha hilo.
Akizungumzia ahadi yake hiyo mwigizaji huyo
mkongwe alisema tayari ameshaitimiza kwa kutayarisha filamu iliyohusisha
mikoa minne na Zanzibar akishirikiana na wasanii wa ndani na nje ya
nchi.
Aliitaja miji ambayo amefanyia filamu hiyo mpya
aliyoipa jina la ‘Mzee wa Swaga’, kuwa ni Visiwani Unguja, Mwanza,
Arusha, Dodoma na Dar es Salaam.
Alisema katika kuhakikisha filamu hiyo aliyoiandaa
kama zawadi ya kufungia mwaka kwa Watanzania inakuwa bora,
aliwashirikisha waigizaji mahiri akiwamo mwigizaji bora wa Zambia Keith
Kabwita, mwigizaji bora wa Zanzibar, Kheri Chimbeni, mkongwe Misayo
Ndumbagwe maarufu Thea, Wastara Juma na Welu Sengo.
Alieleza kuwa lengo la kukusanya vipaji hivyo na
kuzunguka navyo katika mikoa yote hiyo ni kuhakikisha wanapata fursa ya
kuona rasilimali zilizopo nchini, pamoja na kujifunza namna ya kutafuta
fursa kupitia tasnia hiyo ya filamu.
“Mwongozo wa filamu hiyo ambayo naamini mashabiki
wakiiona wataniona nikiwa katika mtazamo mwingine kabisa, ulikuwa
unanilazimu kuhama kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na nikifika katika
mkoa husika natakiwa kukutana na mwenyeji wangu ambaye naye anaingia
moja kwa moja katika filamu,” alisema JB.
Alieleza kuwa ana furaha kubwa kukamilisha zawadi hiyo ya Watanzania na kutimiza ahadi aliyowapa mashabiki wake kuwa, ipo siku atakutanisha waigizaji wa baadhi ya mikoa na kubadilishana uzoefu.
Alieleza kuwa ana furaha kubwa kukamilisha zawadi hiyo ya Watanzania na kutimiza ahadi aliyowapa mashabiki wake kuwa, ipo siku atakutanisha waigizaji wa baadhi ya mikoa na kubadilishana uzoefu.
“Unaona mchanganyiko huo, kaa mkao wa kula filamu
ni kwa ajili ya mashabiki wangu na mapema mwezi ujao itakuwa hewani,”
alisema JB.
Mwigizaji huyo mahiri anayefanya vizuri zaidi
akisimama katika filamu na King Majuto, aliitaja sababu inayomfanya
awaachie waigizaji chipukizi kufanya kazi badala ya kung’ang’ania
kuigiza katika kila filamu anayotayarisha, kuwa ni kujaribu kupanua wigo
wa waigizaji nchini.
Alisema kabla yao kulikuwa na kina mzee Kipara,
Pwagu na Pwaguzi, Mama Ambiliki, Mzee Jongo, Bi Nyakomba, lakini kwa
sababu waliwapa nafasi vijana, hata walipokaa pembeni kwa sababu moja au
nyingine, walimudu kuendeleza walipoachia.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment