Monday, December 8, 2014

Membe achukua tahadhari ya escrow

Bagamoyo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amezindua mfuko wa elimu wa kusomesha wanafunzi waliofaulu kwenda vyuo vikuu lakini familia zao hazina uwezo katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) huku akichukua hadhari dhidi ya kupokea “fedha kama zile za Akaunti ya Tegeta Escrow”.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.PICHA|MAKTABA

Akiutangaza mfuko huo utakaojulikana kwa jina la ‘Bernard Membe Scholarship, waziri huyo aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho, alisema fedha za kuutunisha zitakuwa zinapatikana kupitia harambee na wafadhili.
Hata hivyo, alisema: “Mfuko huu utakuwa ni wa wazi na fedha zote zitakazoingia ni lazima zijulikane zimetoka wapi, ili tusije tukaingia mkenge wa kupata fedha kama za escrow zikatumika kumsomesha mwanafunzi, mwishowe atajisikiaje?”
Akaunti ya escrow kwa sasa ndiyo ‘habari ya mjini’ na Rais Jakaya Kikwete anasubiriwa kutekeleza maazimio ya Bunge yanayoeleza jinsi ya kuwawajibisha baadhi ya mawaziri na watendaji wengine waliohusishwa na uchotaji wa Sh306 bilioni katika akaunti hiyo iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Akaunti hiyo ilifunguliwa ili kuhifadhi fedha za malipo ya gharama za uwekezaji kutokana na mgogoro baina ya Tanesco na IPTL lakini kabla ya uamuzi wa nani mmiliki halali kutolewa, fedha hizo zilichotwa i. Kutokana na kitendo hicho, uchunguzi ulifanyika na Bunge kuazimia baadhi ya vigogo wawajibishwe ama kwa kutoa uamuzi au kupokea sehemu ya fedha hizo.

Mahafali
Akiwatunuku wahitimu 90 wa shahada ya uzamili, shahada ya kwanza, diploma na cheti katika mahafali ya pili ya UB katika viwanja vya Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mwishoni mwa wiki, Membe alisema amebaini kuna tatizo kubwa la ukosefu wa fedha za kusomesha wanafunzi vyuo vikuu na wengi wameacha kwa kukosa uwezo, hivyo mfuko wake utawasomesha.
Alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu anaamini elimu ni rasilimali na urithi wa pekee katika maisha ya binadamu hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
Alisema vijana wanahitaji kupata elimu ya juu lakini familia zao hazina uwezo wa kulipa ada, hivyo mfuko wake aliouanzisha utawapa nafasi ya kuwasilisha maombi na wahusika wakiridhishwa na vigezo, watasomeshwa .
Aliwaomba watu wote wenye uwezo, kuchangia mfuko huo ili vijana wote nchini wanaohitaji elimu lakini hawana uwezo wapate fursa hiyo. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Costa Mahalu alimshukuru Membe kwa uamuzi huo na kusema hata bodi ya mikopo nchini haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaohitaji mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.
Kenyatta
Katika tukio jingine, Membe amempongeza Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kufutiwa kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, (ICC) iliyopo The Hague, Uholanzi. Mwishoni mwa wiki, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda aliondoa kesi dhidi ya Kenyatta akisema amekosa ushirikiano wa Serikali ya Kenya.
Nyongeza na Ibrahim Yamola.Bagamoyo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amezindua mfuko wa elimu wa kusomesha wanafunzi waliofaulu kwenda vyuo vikuu lakini familia zao hazina uwezo katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) huku akichukua hadhari dhidi ya kupokea “fedha kama zile za Akaunti ya Tegeta Escrow”.
Akiutangaza mfuko huo utakaojulikana kwa jina la ‘Bernard Membe Scholarship, waziri huyo aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho, alisema fedha za kuutunisha zitakuwa zinapatikana kupitia harambee na wafadhili.
Hata hivyo, alisema: “Mfuko huu utakuwa ni wa wazi na fedha zote zitakazoingia ni lazima zijulikane zimetoka wapi, ili tusije tukaingia mkenge wa kupata fedha kama za escrow zikatumika kumsomesha mwanafunzi, mwishowe atajisikiaje?”
Akaunti ya escrow kwa sasa ndiyo ‘habari ya mjini’ na Rais Jakaya Kikwete anasubiriwa kutekeleza maazimio ya Bunge yanayoeleza jinsi ya kuwawajibisha baadhi ya mawaziri na watendaji wengine waliohusishwa na uchotaji wa Sh306 bilioni katika akaunti hiyo iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Akaunti hiyo ilifunguliwa ili kuhifadhi fedha za malipo ya gharama za uwekezaji kutokana na mgogoro baina ya Tanesco na IPTL lakini kabla ya uamuzi wa nani mmiliki halali kutolewa, fedha hizo zilichotwa i. Kutokana na kitendo hicho, uchunguzi ulifanyika na Bunge kuazimia baadhi ya vigogo wawajibishwe ama kwa kutoa uamuzi au kupokea sehemu ya fedha hizo.
Mahafali
Akiwatunuku wahitimu 90 wa shahada ya uzamili, shahada ya kwanza, diploma na cheti katika mahafali ya pili ya UB katika viwanja vya Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mwishoni mwa wiki, Membe alisema amebaini kuna tatizo kubwa la ukosefu wa fedha za kusomesha wanafunzi vyuo vikuu na wengi wameacha kwa kukosa uwezo, hivyo mfuko wake utawasomesha.
Alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu anaamini elimu ni rasilimali na urithi wa pekee katika maisha ya binadamu hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
Alisema vijana wanahitaji kupata elimu ya juu lakini familia zao hazina uwezo wa kulipa ada, hivyo mfuko wake aliouanzisha utawapa nafasi ya kuwasilisha maombi na wahusika wakiridhishwa na vigezo, watasomeshwa .
Aliwaomba watu wote wenye uwezo, kuchangia mfuko huo ili vijana wote nchini wanaohitaji elimu lakini hawana uwezo wapate fursa hiyo. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Costa Mahalu alimshukuru Membe kwa uamuzi huo na kusema hata bodi ya mikopo nchini haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaohitaji mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.
Kenyatta
Katika tukio jingine, Membe amempongeza Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kufutiwa kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, (ICC) iliyopo The Hague, Uholanzi. Mwishoni mwa wiki, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda aliondoa kesi dhidi ya Kenyatta akisema amekosa ushirikiano wa Serikali ya Kenya.

No comments:

Post a Comment