Hii ni ya yule mtu aliyekuwa anashikilia rekodi ya kuwa mtu mnene kuliko wote Duniani …

Rekodi mbalimbali zimekuwa zikivunjwa
kila siku Duniani, siku chache zilizopita tuliisikia ile ya watu wawili
waliovunja rekodi mbili kubwa ile ya mtu mfupi kuliko wote na mtu mrefu
kuliko wote Duniani kukutana kwa mara ya kwanza.
Leo kuna taarifa kuhusu mtu aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mnene kuliko wote duniani kwa kuwa na uzito wa Kilo 444, Keith Martin ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 44.
Wakati wa uhai wake aliwahi kufanywa
upasuaji na robo tatu ya nyama za kwenye tumbo lake ilikuwa imeondolewa
na kufanikiwa kumpunguza nusu ya uzito wa mwili wake, ambapo kifo chake
kimetokea miezi nane toka afanyiwe upasuaji huo kwa kuugua ugonjwa wa
Pneumonia.
Kabla ya upasuaji Martin alikuwa anakula
Calories 20,000 kiasi ambacho ni mara kumi ya kiasi ambacho
kinapendekezwa kuliwa na mtu mzima.
Moja ya vitu alivyopendelea kula wakati wa kifungua kinywa ni Pizza
na Mayai na kutokana na tatizo la uzito mkubwa Martin aliwahi kukaa
ndani ya nyumba yake huko Uingereza kwa miaka 10 bila kutoka nje
kutokana na kuelemewa na uzito mkubwa.Moja ya dada zake amesema wana majonzi kumpoteza ndugu yao na bado wanaendelea kuomboleza msiba huo.



Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza
No comments:
Post a Comment