Sunday, December 7, 2014

Hawa ndiyo mastaa waliotajwa kwenye vipengele vingi zaidi tuzo za Grammy 2015

grammy-54th-poster-frank-gehry-272Wiki hii imetajwa ile list ya mastaa ambao wanawaniwa tuzo za Grammy zitakazofanyika February 2015, kitu kizuri kwenye list hii ni kwamba kuna mastaa  ambao wametajwa kuwania vipengele vingi zaidi kuliko mastaa wengine wote.
Mwandishi na mwimbaji Sam Smith, mama wa Blue Ivy na mke wa Rapper Jay Z, Beyonce na mkongwe asiyezeeka ambaye ni mtayarishaji wa muziki na mwimbaji pia Pharrell Williams wametajwa kuwa ni wasanii ambao wametajwa kuwania tuzo nyingi zaidi kwenye Tuzo za  Grammy zitakazofanyika February mwaka 2015.
sam-smith-beyonce-pharrell
Mastaa hao wametajwa kuwania kwenye vipengele sita kila mmoja huku masikio na macho ya wengi yakiangalia nani kati yao ataweza kuivunja ile rekodi ya kubeba tuzo zote sita?
Unahitaji kutopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu? Ni rahisi sana, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter  na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Facebook

No comments:

Post a Comment