Daktari feki akamatwa Tanzania
Sekta ya afya nchini Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la madaktari fekiambapo jana Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu, MOI ilimkamata daktari feki aliyefahamika kwa jina la Dismas John Macha mwenye umri wa miaka 35.
Taasisi hiyo ipo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, MNH jijini Dar es Salaam, ambapo daktari huyo anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa madai kwamba angemhudumia mgonjwa wao.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamatwa kwamtuhumiwa huyo, Mkurugenzi wa MOI, Athumani Kiloloma, alisema maraya kwanza alikamatwa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, akijifanya mwanafunzi wa shahada ya uzamili katikashule ya tiba.
Dk. Kiloloma alisema alipokamatwa mara ya kwanza, walitoa matangazo katika hospitali nzima na kutoa taarifa kwa wananchi, lakini wanashangaa tukio hilo limejirudia tena.
Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la madaktari feki, ambao wamekuwa wakiomba michango mbalimbali ya fedha.
Mtuhumiwa Dismas Macha anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibumashitaka yanayomkabili.
Awali, Dismas akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye sidaktari bali ni mgonjwa wa akili.
Matukio ya madaktari feki yamekuwa yakiripotiwa katika hospitalimbalimbali nchini Tanzania katika siku za karibuni, ambapo inadaiwa madaktari hao kazi kubwa ni kuwatapeli wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.
MONDAY, DECEMBER 8, 2014
Yaya aliyemtesa mtoto UG aomba msamaha
Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto
Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.
No comments:
Post a Comment