Chanjo ya EBOLA yatoa matumaini
Watafiti wa masuala ya afya nchini MAREKANI, wamesema, majaribio ya
chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA yaliyofanyika nchini humo,
yanaonekana kuwa ya mafanikio.
Chanjo hiyo imetengenezwa ili kuchochoea kinga ya mwili wa binadamu
ili itengeneze kinga dhidi ya virusi vya EBOLA. Watafiti hao wanasema
chanjo hiyo imeonyesha mafaniko, kwa vile watu waliokubali kufanyiwa
majaribio, miili yao imeweza kutengeneza kinga dhidi ya EBOLA katika
kipindi cha wiki nne.
Utafiti huo unaonyesha kuwa watu waliofanyiwa majaribio ya chanjo
dhidi ya EBOLA, hawakupata athari hasi za chanjo hiyo. Taasi
inayoshughulika na chanjo hiyo, inatarajiwa kufanya majaribio zaidi
kuhusiana na chanjo hiyo mwezi ujao.
Kajaribio ya awali ya chanjo hiyo yanatarajiwa kufanyika nchini LIBERIA, ambako watu wengi wameathiriwa na EBOLA.
No comments:
Post a Comment