Wednesday, December 31, 2014


Move Ya Jutta Schuhn Rock Divas Jutta Schuhn


Move ya! toning / workout: aerobic music/ fitness music, Aerobic music - musik-onlineshopping bei move ya! - aerobic,music,musik,move,ya,aerobicmusik,aerobicmusic,fitness,shop,music,shop,music,onlinemove ya! aerobic music. Move ya! step / dance: aerobic music/ fitness music chart, Aerobic music - musik-onlineshopping bei move ya! - aerobic,music,musik,move,ya,aerobicmusik,aerobicmusic,fitness,shop,music,shop,music,onlinemove ya! aerobic music.

MOVE YA! TRIBUTE TO DONNA SUMMER





MOVE YA! Calvin Wiley MILKSHAKE Calvin Wiley

How to MOVE YA! Calvin Wiley MILKSHAKE Calvin Wiley

MOVE YA! CHART ATTACK Winter 2013

How to MOVE YA! CHART ATTACK Winter 2013

MOVE YA! TRIBUTE TO DONNA SUMMER

How to MOVE YA! TRIBUTE TO DONNA SUMMER

MOVE YA! Christiane Reiter ReitHOUSE MOVES Vol. 4 // 132BPM

How to MOVE YA! Christiane Reiter ReitHOUSE MOVES Vol. 4 // 132BPM

Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.


                             Picha iliyotumika hapa haihusiani na habari inayoelezwa
Ajira ni kitu kizuri sana, maana kupitia ajira ndio tunapata watu wa kutufanyia kazi mbalimbali na pia kutupatia huduma mbalimbali. Na kuna kipindi ajira ilikuwa kitu muhimu sana kiasi kwamba aliyekuwa na ajira alionekana kuyashinda maisha. Lakini nyakati hizo zimepita sasa na tumeingia kwenye kipindi ambacho ajira zimekuwa na changamoto kubwa sana.

Kwanza nafasi za ajira zimekuwa chache kuliko idadi ya wanaozihitaji hivyo kufanya idadi ya wasiokuwa na ajira kuwa kubwa.

Na pili, hata waliopo kwenye ajira hawaridhishwi na ajira zao kwa maana kwamba wanajikuta wanafanya kazi miaka mingi lakini hawaoni mabadiliko makubwa kwenye maisha yao.

Pamoja na changamoto hizi za ajira, kuna fursa nyingi ambazo zipo nje ya ajira, ila waliopo kwenye ajira na hata wanaotafuta ajira bado hawahangaiki kuzitumia vizuri. Bado mtu atang’ang’ania kufanya kazi aliyoanza kuifanya miaka 10 iliyopita japo hakuna chochote anachoweza kukionesha kwa miaka hiyo kumi zaidi ya madeni na msongo wa kila siku hasa linapokuja swala la fedha.

Jambo hili limenifanya kufanya utafiti wa ndani zaidi ili kujua kwa nini waliopo kwenye ajira hata kama haiwaridhishi hawapo tayari kutafutra fursa nyingine? Na pia kwa nini vijana wanaomaliza masomo yao, wapo tayari kukaa nyumbani mwaka mzima, kuzunguka na bahasha ya kuomba kazi badala ya kufikiria kutumia fursa nyingine?

Katika kulitafiti hilo nimegundua mbinu mbili ambazo waajiri wote wanazitumia kuhakikisha waajiriwa wanaendelea kuwa watumwa wao. Naposema watumwa, iko wazi kwamba kama mtu anafanya kazi ambayo haimridhishi na wala haifurahii hakuna neno rahisi la kutumia zaidi ya utumwa.

Mbinu hizi mbili zimetumiwa vizuri sana na waajiri na zimeingia kwenye akili ya waajiriwa kiasi kwamba ni vigumu sana kunasua kwenye mtego walioingia.

Mara nyingi unakutana na mtu anayeanza ajira na anakuambia atafanya kwa miaka kadhaa na baadae ataacha afanye mambo mengine makubwa, ila kadiri miaka inavyozidi kwenda ndivyo anavyozidi kuwa na hofu ya kuacha ajira ile. Hii yote inatokana na mbinu hizi zilizotengenezwa na waajiri.

Mbinu ya kwanza; Kuwashawishi kwamba kupitia ajira ndio wataweza kumudu maisha yao.

Kupitia mbinu hii waajiri wanawafanya waajiriwa kuamini kwamba kupitia ajira ndio wanaweza kuyamudu maisha yao. Wanafanya hivi kwa kumhakikishia mfanyakazi mshahara wake wa mwezi, iwe kampuni au taasisi imefanya kazi kwa faida au la. Mfanyakazi hata kama ana mshahara mdogo kiasi gani ana uhakika wa kuupata kila inapofika mwisho wa mwezi.

Pia kupitia mbinu hii waajiri wanawahakikishia wafanyakazi wao maisha mazuri hata baada ya kustaafu. Wanawachangia katika mfuko wao wa mafao ya uzeeni na pia mfuko huu unawafanya waajiriwa kuona kuna kitu kizuri na kikubwa mbeleni, hivyo kuendelea kuwa wafanyakazi watiifu.

Mbinu ya pili; Kumwogopesha mwajiriwa kwamba hakuna maisha nje ya ajira.

Kupitia mbinu hii waajiri wameweka sheria mbalimbali ambazo zinamfanya mwajiriwa aendelee kuwa mtumwa kwa mwajiri wake. Kwa mfano mwajiriwa ameshakaa kwenye ajira kwa miaka kumi na ameshachangia kiasi kikubwa kwenye mafao yake, ataambiwa akiacha kazi au kufukuzwa kazi mafao yake, ama anayapoteza au atayadai akishafikisha umri halali wa kustaafu. Hiki ni kifungo kikubwa sana kinachomhakikishia mwajiri kwamba anaendelea kuwa na watu wanaomtumikia hata kama hawataki kufanya hivyo.

Mbinu hizi mbili zimeshaingia kwa wafanyakazi ambao ni wakongwe kazini na ndio maana wengi wanaweza kupanga kuacha kazi na kufanya mambo mengine lakini wanashindwa. Swali la kushangaza ni je mbinu hizi mbili zimepandikizwaje kwa vijana ambao bado hawajaingia kwenye ajira kabisa?

Kwa vijana ambao bado hawajaingia kwenye ajira kabisa nao wameshanasa mtego huu. Wameshaoneshwa kwenye ndoto kwamba kupata ajira kwanza ndio kujiwekea usalama wa maisha na hata kama ni kuangalia fursa nyingine basi ni baada ya kuwa kwenye ajira kwanza. Hivyo wanakazana kuingia, wakifikiri wataweza kutoka watapotaka, ila wakishanasa mtego wanaishia kuwa watumwa kwa kipindi kirefu kwenye maisha yako.

Unahitaji maarifa na nguvu ya ziada ili kunasua kwenye mtego huu. Unahitaji kuangalia uhalisia ili uweze kujua kwamba lolote linawezekana iwe ni kwenye ajira au nje ya ajira. Na unahitaji uweze kufanya maamuzi yako mwenyewe, kuyasimamia na kutokusikiliza wanaokukatisha tamaa ndio utaweza kuondoka kwenye mtego huu.

Vinginevyo utakuwa unaweka mipango kila siku ya kujikomboa lakini ikifika kuchukua maamuzi, unajikuta upo kwenye mtego aliokuwekea mwajiri wako.

Mwaka 2014 umeisha, je umefanya nini? Umefikia malengo uliyopanga? Na je umejipangaje kwa mwaka 2015? Karibu kwenye semina ya siku 21 za mafanikio makubwa mwaka 2015 itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina hii itakuwezeshakuweka malengo ambayo utaweza kuyafikia, kubadili fikra mbaya ulizopandikizwa zinazokufanya uendelee kuwa mtumwa na pia kukupa mbinu za kuboresha kazi au biashara unayofanya. Kushiriki semina hii andika email kwendaamakirita@gmail.com


Meli vita ya Indonesia KRI Yos Sudarso  moja ya meli kadhaa zinazoshiriki usakaji wa ndege ya AirAsia .

WATAALAMU wanaosaka ndege ya AirAsia yenye mruko namba QZ8501 wamesema wameona mabaki ya ndege hiyo kwa kutumia utaalamu wa kusikia mshindosauti (sonar) chini ya bahari ya Java.
Hata hivyo taarifa waliyoitoa dakika 40 zilizopita wamesema kwamba hawana uhakika kama ndege hiyo ipo nzima au ni kipande tu kimeonekana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ndugu wa abiria waliokuwapoi katika ndege hiyo wametaarifiwa kuonekana kwa mabaki hayo.
Awali jana watafutaji hao waliona sehemu ya mabaki yakielea.
Aidha maiti kadhaa zilizpatikana jana.
Mabaki hayo yalipatikana  umbali wa kilomita 100-200 kutoka eneo la mwisho ambalo rubani alifanya mawasiliano ya kutaka kubadili njia.

Tuesday, December 30, 2014

MUME AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA HAWARA WA MKE WAKE BAADA YA KUWAFUMANIA



Mkazi wa Tarafa ya Mang’ula wilayani Kilombero mkoani Morogor, Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa kwa kisu na anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo.
Tukio hili lilitokea usiku wa Desemba 23 huko Mang’ula na inadaiwa kuwa marehemu alirudi nyumbani saa 3.30 usiku na kumkosa mkewe hivyo kuamua kumtafuta katika maeneo mbalimbali.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mang’ula, Shabani Lichaula na Mkuu wa kituo cha Polisi Mang’ula, Nkilijia Lazaro walisema polisi inamshikilia mke huyo mdogo wa marehemu huku likimtafuta mtuhumiwa.
Lichaula alidai kuwa marehemu katika kumtafuta mkewe huyo alimkuta akiwa amesimama mahali na mwanamume na mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu Nyenja aliamua kumvaa mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni hadi utumbo kutoka nje.
Lichaula alisema baada ya Nyenja kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema walijitokeza na kumpeleka Kituo cha Afya Mang’ula.
Mganga Mkuu wa Mang’ula, Eugen Shirima alisema baada ya huduma ya kwanza walimpatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Mtakatifu Francis, Ifakara kwa matibabu lakini alifariki dunia wakiwa njiani.

Na Lilian Lucas, Mwananchi 

Story ya mwanamke anayelaza waume za watu kwenye Pub yake, #Hekaheka ya December 30

Gone to the PubHekaheka iliyosikika kwenye show ya Leo Tena ya Clouds FM, imetokea Mbezi, Dar es Salaam.
Wanawake wawili wamelalamikia kitendo cha dada mmoja ambaye amefungua pub ya kuuza vinywaji, lakini wanawake hao wamesema kuwa mwanamke huyo ameweka magodoro mawili ambapo ametuhumiwa kuwa anawalaza wanaume za watu ndani ya Pub hiyo.
Mwanamke mmoja amesema kuwa waliuza nyumba na mumewe na wakaamua kujenga nyumba nyingine lakini mwanaume huyo alimtelekeza mkewe eneo la ujenzi na kwenda kunywa pombe katika Pub hiyo, alipomfuata mwanaume huo aligoma kuondoka hivyo mwanamke akaamua kumwaga vinywaji vilivyokuwa kwenye meza na kupelekea ugomvi kati yao.
Wanawake hao waliandamana kwenda kwenye Pub ya mwanamke huyo ili wakamseme kuhusu tabia hiyo, lakini mwanamke huyo alikataa kuwa huwa anawalaza wanaume hao katika Pub yake, ila magodoro ambayo yapo huwa wanayatumia wafanyakazi wake kulala wakati wa usiku.

Monday, December 29, 2014

Kinachoendelea hivi sasa kuhusu ndege iliyopotea jana Indonesia

majonzi
Taarifa zilizotoka muda mfupi uliopita kuhusiana na zoezi la utafutaji wa ndege iliyopotea ya Asia QZ 8501 zinasema kuwa vikosi vinavyohusika na utafutaji wa ndege hiyo vinasema kuna uwezekano mkubwa imezama kwenye kina kirefu cha bahari.
Chanzo cha habari kutoka nchini humo kinasema uchunguzi kuhusu ndege hiyo bado unaendelea huku wakitumia ndege za kijeshi kutoka Indonesia na Singapore Kusini Magharibi  mwa Pwani ya Borneo ambapo ilipoteza mawasiliano.
kapt
Kapteni wa ndege hiyo Iriyanto
Bado jitihada za kuwatafuta abiria 162 waliokuwepo ndani ya ndege zinaendelea,na mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote,ilikua ikielekea Singapore.
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia na shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
air
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

Hili ni dili analofungia mwaka 2014 msanii Davido…

DavidO (1)Mwezi December ni mwezi ambao watu huwa wanafanya uchambuzi wa namna mwaka ulivyokwenda, kuangalia malengo ambayo umeyaweka yamepita au yamekwama na pia kuandaa mikakati mipya ya mwaka unaofuatia.
Davido ni mmoja ya mastaa wanaomaliza vizuri 2014, amefanya vizuri kwenye muziki, siku ya December 27 alitoka na tuzo mbili kwenye AFRIMA Awards 2014, msanii Bora wa Mwaka na pia Hit Single yake ya ‘Aye’ kuwa wimbo bora wa mwaka.
JUST SIGNED A DEAL WITH CLOSE UP! GREAT WAY TO END THE YEAR!! NON STOP THANK YOU LORD!! #owonikoko”– @davidoofficial
Hizo ni dalili njema kwa Davido 2015, tayari amesign dili ya kutangaza dawa ya mswaki ya Close Up hivyo mbali na mauzo ya album aliyopanga kuitoa mwakani pamoja na deal nyingine ikiwemo ya shows, kupitia hii kajihakikishia mkwanja wa kutosha 2015.
dav

Hili ni dili analofungia mwaka 2014 msanii Davido…

DavidO (1)Mwezi December ni mwezi ambao watu huwa wanafanya uchambuzi wa namna mwaka ulivyokwenda, kuangalia malengo ambayo umeyaweka yamepita au yamekwama na pia kuandaa mikakati mipya ya mwaka unaofuatia.
Davido ni mmoja ya mastaa wanaomaliza vizuri 2014, amefanya vizuri kwenye muziki, siku ya December 27 alitoka na tuzo mbili kwenye AFRIMA Awards 2014, msanii Bora wa Mwaka na pia Hit Single yake ya ‘Aye’ kuwa wimbo bora wa mwaka.
JUST SIGNED A DEAL WITH CLOSE UP! GREAT WAY TO END THE YEAR!! NON STOP THANK YOU LORD!! #owonikoko”– @davidoofficial
Hizo ni dalili njema kwa Davido 2015, tayari amesign dili ya kutangaza dawa ya mswaki ya Close Up hivyo mbali na mauzo ya album aliyopanga kuitoa mwakani pamoja na deal nyingine ikiwemo ya shows, kupitia hii kajihakikishia mkwanja wa kutosha 2015.
dav

Saturday, December 27, 2014

Diamond AWAFUNIKA ALI KIBA NA YUSUPH MLELA KWA MVUTO MWAKA HUU 2014..APOKEA TUZO


Diamond Platnumz has been voted Ijumaa Sexiest Bachelor of 2014. The contest was conducted by Globalpublishers' Ijumaa news paper. more than 30 Tanzanian male celebrities were competing for the title for months.
Ali Kiba, Diamond and Yusuph Mlela entered the final stage and eventually yesterday at Darlive Diamond was announced the winner.

MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI TAMASHA LA UPENDO WA MAMA DAR

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza.

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania. Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.
 Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha. Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi. "...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati
itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi. Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao. 
 Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla. Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.

Friday, December 26, 2014

Wanasayansi wako kazini… Safari hii wametafiti hii ya wanaume kunyonyesha watoto

baby-breastfeedingDunia na maajabu yake kwenye siku nyingine, leo kuna tafiti inayosema kuwa eti wanasayansi wanasema kwa kuangalia vigezo vya kibaiolojia wanaume wanaweza kunyonyesha hivyo huenda muda mfupi ujao jukumu hilo lisiwe la wanawake peke yao.
Dr. Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala amesema mwanaume anaweza kutoa maziwa lakini sio maziwa yafaayo kwa lishe ya mtoto.
… Wapo wanaume wanaochezea chuchu kwa muda mrefu na kufanya hivi wanaweza kusababisha maziwa kutoka…Dk. Semkuya
Daktari mwingine mstaafu anasema hivi;Wanaume wana tezi zao na wanawake wana tezi za kipekee ambazo zinawasaidia kuzalisha maziwa…”— Dk. Malise Kaisi.
Daktari mwingine bingwa wa magonjwa ya binadamu Meshack Shimwela amesema mwanaume anaweza kutoa majimaji katika chuchu zake lakini hayo sio maziwa.
Iliwahi kuripotiwa kuwa mwaka 2002 kulikuwa na mwanaume aliyeamua kumnyonyesha mwanae baada ya kufiwa na mke wake Sri Lanka, lakini story ni kwamba Jarida la Lancet limeeleza kuwa mwanaume anapokaa na mtoto mchanga na kuamua kunyonyesha tezi za maziwa zinazoitwa lobules huzalisha maziwa hivyo kukawezekana mwanaume kunyonyesha maziwa kama ya mwanamke.
Ripoti ya Jarida hilo imesema kwa watu wenye jinsia mbili kuna uwezekano sio wa kunyonyesha tu, bali hata kubeba ujauzito kutokana na mchanganyiko wa homoni.
Comment yako mtu wangu wa nguvu, unadhani ikithibitika hii ya wanaume kunyonyesha hali itakuwaje?
Chanzo cha Habari: Gazeti MwananchiDecember 26.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi

Simba bado kiza kinene.


MASHABIKISIMBA
Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara imerejea hii leo baada ya mapumziko ya mwezi mmoja na nusu wakati ligi hiyo iliposimama .
Katika mchezo uliopigwa hii leo , wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club walianza vibaya nusu ya pili ya mzunguko wa kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao moja bila .
Bao hilo pekee lilifungwa kwenye dakika ya 21 na  mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union Atupele Green ambaye alifanyia kazi makosa ya kipa wa Simba Ivo Mapunda na beki Mohamed Hussein .
Kwa matokeo haya Kagera Sugar wamefikisha pointi kumi na tatu baada ya michezo nane na wanapanda mpaka kwenye nafasi ya nne .
Ligi hiyo itaendelea hapo kesho kwa michezo miwili ambapo Jkt Ruvu na Ruvu Shooting watacheza huko Azam Complex Chamazi , na Tanzania Prison watacheza na Coastal Union huko Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.

SUPERSTAR WA BONGO MOVIE AFUMANIWA NA MKE WA MTU NA HIKI NDICHO ALICHOFANYIWA



Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Christmass duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa wakristo wote kuzaliwa kwa Mwokozi wao "YESU" Wengine siku hiyo wanaifanya kuwa siku ya starehe na kufanya mambo kinyume na maana ya siku yenyewe. Msanii wa filamu za bongo maarufu kwa jina la Pancho Mwamba, anadaiwa kufanyiwa mbaya baada ya fumanizi siku ya Xmass. Msanii huyo inasemekana amefumaniwa na mke ambaye si wake siku ya Christmass maeneo ya Kinondoni jijini hapa
Patcho Mwamba Lukusa ni muimbaji, Mtunzi, Composer, Music 
Arranger, Mchezaji, Mchekeshaji na ni muigizaji wa 
cinema. Patcho amejitokeza kucheza vizuri katika tasmia nzima ya 
sinema huku ajijizolea umaarufu kama mwanamuziki huyu toka 
kundi la FM Academia wana Ngwasuma ameweza kujizolea sifa kem kem toka kwa mashabiki wa Dollywood

Thursday, December 25, 2014

 
Staa wa sinema Bongo, Rose Ndauka akifurahia jambo.

MASTAA wa sinema waliowahi kuwa wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa kurudiana na hivi sasa ni mapenzi motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose na Richie wamedaiwa kurudiana baada ya mwanadada huyo kumwagana na mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi ya hivi karibuni.

“Hivi nyie wadaku mnajua Rose Ndauka na Richie sasa hivi ni mahaba niue kama zamani? Wamekuwa wakigandana na mara nyingine hupatikana maeneo ya Bahari Beach (jijini Dar) kiasi kwamba wasanii wenzao tunawashangaa.

“Inaonekena walipomwagana hakuna aliyekuwa tayari,” alisema msanii mmoja wa filamu za Bongo ambaye aliomba jina lake kusokomomezwa kwenye makabrasha ya gazeti hili.Baada ya kuzinyaka habari hizo, Amani lilimtafuta Richie kwa njia ya simu ya mkononi ili aeleze chochote kuhusu madai hayo.


Staa wa sinema Bongo, Single Mtambalike ‘Richie’ akipozi.
“Unaposema tumerudiana una maana gani? Mimi sijawahi kuwa na uhusiano na Rose Ndauka itakuwaje sasa turudiane? Hakuna kitu kama hicho, mimi na Rose tulikuwa tunacheza filamu ambayo nilimshirikisha na tumemaliza.

“Halafu sikia wewe, mimi si mtu wa magazeti na endapo mtaandika hii habari nitamfanyia mtu ‘kitumbaya’ hadharani maana ninyi mnatafuta habari za uongo ili mpate fedha.”

Baada ya Amani kumalizana na Richie, lilimsaka Rose Ndauka ambaye naye aliruka kimanga:
“Ha! Ha! Mimi sijarudiana na Richie, tulikuwa tunacheza filamu moja ndiyo maana muda mwingi tulionekana kuwa wote. Lakini filamu yenyewe tumeshamaliza.”

Wednesday, December 24, 2014

TAWI LA CCM NEW YORK YA PATA KATIBU WAKE RASMI BWANA STEVE BUBE

 Tarehe 13/12/2014 ccm tawi la NY limepata katibu mpya Steve Bube na katibu mwenezi ni Gaston Mkapa.

TANGAZO…………… TANGAZO…………………………TANGAZO.


KAMPUNI YA SMART COMMUNICATION GENERAL ENTERPRISE LTD (SCGE) inapenda kukukaribisha katika usiku wa kihistoria wa zawadi maalum kwa wanandoa utakaoweka historia mpya tangu kuanza kwa ndoa yako.
Siku hii maaluma ya kukumbukwa itakuwa tarehe 26/12/2014 yaani siku ya Chrismas Box ambayo watu wote duniani huitumia kwa ajili ya kupeana zawadi, Lakini wewe siku hiyo utaitumia kwa ajili ya kupeana zawadi kwa mwandani wako ndani ya Ukumbi wa Mkapa kuanzia saa 12 jioni.
Siku hii itapambwa na burudani kabambe za muziki wa aina mbali mbali utakaowafanya mjisikie kutojutia kuwa ndani ya ndoa, pia kutakuwa na mafundisho kwa Walimu wa NDOA waliobobea ambao watakueleza nini maana ya ndoa, faida zake, furaha ya ndoa, siri ya ndoa inayodumu miaka mingi  na mengine mengi.
Pia kutakuwa na chakula kizuri na vinywaji, njoo na mwenzi wako ambapo viongozi mbali mbali na watu maarufu wakakuwepo wakiwemo viongozi wa serikali katika Mkoa wa Mbeya.
Ili kufanikisha maandalizi na usiku huu wa ajabu kwako unaombwa kuchangia shilingi elfu hamsini(50,000/= tu )
Mungu akubariki na ahsante kwa utayari wako, njoo tufurahi pamoja na kujua  mpango wa Mungu kwa wanandoa.
Kwa mawasiliano zaidi;
Charles Mwakipesile (Mratibu mkuu) 0754- 301848
Au Mtumuli 0755- 367723.

Uwendawazimu wetu, ufisadi na wafadhili

 Si uchochezi kusema kuwa watawala wetu wameshindwa, tena vibaya sana. Ni aibu kwa taifa ambalo limesherehekea miaka 53 ya uhuru kushindwa kufanya maamuzi magumu hadi lishinikizwe na wafadhili. Tishio na amri ya hivi karibuni toka kwa serikali ya Marekani kwa Tanzania kuwa haitatoa fedha za Changamoto za Milenia (MCC) kama serikali haitawachukulia hatua watuhumiwa wa kashfa ya uchotaji wa mabilioni ya fedha za umma, escrow ni somo tosha.
          Heri wafadhili wamenena. Hili ni pigo na aibu kwa rais Jakaya Kikwete, serikali na CCM ambao wamekuwa wakiwahadaa watanzania kuwa wako madarakani kwa maslahi yao wakati hali ni tofauti. Huu ni ushahidi kuwa CCM na serikali yake wamewekwa mfukoni na mafisadi. Hali ikiendelea hivi, watawala wetu wataipeleka nchi kubaya. Huu ni ushahidi tosha kuwa utawala wa sasa umechoka, upumzishwe ili wenye uwezo watawale na kusafisha uchafu uliopo. Inakuwaje wananchi wanashindwa kuona haya na kuiwajibisha vilivyo CCM kwa kuishikisha adabu?
          Ni ajabu kwa nchi inayojidai kuwa na utawala wa sheria lakini ikawekwa mifukono mwa matapeli wachache, wasaka tonge na wahalifu wa kawaida. Ziko wapi tambo za kupambana na biashara ya madawa ya kulevya? Nani anawagusa? Je hawa hawana ubia kwenye serikali ya sasa? Je hawa hawajaiweka serikali mfukoni? Asitokee mtu akaniambia kuwa hawajulikani. Mbona rais alishakiri kupewa orodha ya wauza unga asiifanyie kazi kwa sababu ajuazo? Je inakuwaje tunashindwa kupambana na ufisadi ilhali tukijua kuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa? Je ni kwa vile mafisadi ni washirika wa nyuma ya pazia ya watawala wetu?
          Najua wengi wanaweza kusema tunaizushia serikali.  Kama watachunguza sababu za serikali kuruhusu ufisadi kuwa sehemu ya maisha ya serikali yetu, wataelewa tunachosema. Hivi kweli nchi inayoamriwa na wafadhili la kufanya ni huru? Je kwa uzembe na upofu wetu tunapaswa kuwalaumu wafadhili kwa kuingilia mambo yetu? Watashindwaje kuingilia iwapo tunafanya mambo ya kitoto na ya hovyo? Imefikia mahali hata bunge linatoa maagizo halafu wakubwa wanayadharau na kuja na mambo yasiyo ingia kichwani kama ilivyotokea juzi wakati Ikulu iliposema kuwa haitawawajibisha watuhumiwa wa wizi wa escrow wala kuchukua hatua hadi ifanye uchunguzi wake. Tambo za ikulu zimeishia wapi baada ya kubanwa? Ndani ya wiki moja ikulu, ikiwa imechanganyikiwa na kujichanganya ilitoa tamko jingine la kijichanganya zaidi ikisema kuwa rais atawashughulikia watuhumiwa ndani ya wiki moja. Hii maana yake ni kwamba ikulu imeminywa na kufanya kile ambacho haikutaka kufanya. Maana ukiangalia timing ya tamko la Marekani na mkengeuko wa Ikulu unagundua kuwa hata kama rais atawawajibisha wahusika si kwa kutaka bali kulazimishwa na wafadhili. Je rais au chama kinachounda serikali vya namna hii bado vinawafaa watanzania? Je ni vibaya kusema kuwa rais amegeuka mhimili wa ufisadi anaopaswa kuuchikia na kupamba nao? Je ni kwanini inakuwa hivi kama rais hanufaiki na jinai hii au kuishiriki?
          Ushahidi wa kimazingira unaonyesha wazi kuwa, kama si papara za bunge, au tuseme kuwekwa sawa na kuingia mkenge, lilipaswa kuiwajibisha serikali yote. Kwa vile inaonyesha escrow ni dili lao. Haiwezekani mawaziri tena waandamizi na maafisa wengi wa serikali waruhusu wizi wa mabilioni hivi kusiwe na mkono wa wakubwa zao. Nani anakanusha kutajwa kwa afisa wa ikulu Prosper Mbena anayedaiwa na kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa aliandika barua ya kushinikiza pesa zichotwe? Je hapa tunatafuta ushahidi upi wa kuihusisha ikulu? Ushahidi mwingine ni ukimya wa muda mrefu wa serikali. Hata kitendo cha rais kusuasua hadi alazimishwe na wafadhili kuchukua hatua ni ushahidi tosha ukiachia mbali rais kuhusishwa moja kwa moja na uletaji wa kampuni jizi ya IPTL hapo mwaka 2004.
          Laiti wafadhili wangekwenda mbele zaidi na kuhakikisha hili jinni linalotunyonya damu IPTL linafurushwa na wahusika kufungwa, wangekuwa wametukomboa hata kama wakubwa watalalamika kuwa wanaingiliwa. Kwanini wasiingiliwe iwapo wamejirahisi kiasi cha kuacha mafisadi wajifanyie watakavyo? Kwanini wasiingiliwe iwapo wameonyesha wazi walivyo wa hovyo na fisadi? Nani angeweza kumwamrisha baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere katika lolote? Je ilikuwaje Nyerere akaogopewa na kutopewa amri? Jibu ni rahisi. Alikuwa msafi na mwenye visheni tofauti na hawa walioigeuza ikulu deni la wezi kama alivyowahi kuonya Nyerere huku akiwakataa wengi wa tunaowaona leo madarakani wakiyafuja ili kutimiza utabiri na madai ya nguli huyu (Mungu amlaze pahali pema peponi). Rais anayeamrishwa kufanya alichoapa kufanya amebaki na nini? Je nafsi zo zinawasuta? Je sisi tunawasuta na kuwawajibisha au kuendelea kuwagwaya?
          Tumalizie kwa kuwataka watanzania kutorudia makosa. Kwenye uchaguzi ujao licha ya kuhoji ni kwanini ufisadi uliachiwa kuwa sehemu ya utawala wasiangalie sura wala ukongwe wa chama. Wahakikishe wanajipatia serikali safi, mpya, yenye mapya na si huu wendawazimu wa siku zetu. Maana waingereza husema “insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results.” Tuachane na wendawazimu huku tukijitofautisha na mafisadi ili mataifa mengine yasiendelee kutucheka kwa kuruhusu taifa letu kuwa shamba la bibi tena bibi mwenyewe hamnazo. Imetosha, wananchi wanapaswa kuanza kwajibika kwa kuwawajibishwa watawala fisadi na wachovu na wabovu.
Chanzo: Tanzania Daima leo.

Amwacha mumewe na dadake uchi barabarani

Mwanamke kwa jina Ting Su nchini Uchina alimwacha mumewe na dadake bila nguo barabarani baada ya kuwapata wakifanya mapenzi Ting Ting Su aligundua kwamba mumewe alikuwa akimdanganya na dadaake na kuwafuata hadi katika kituo kimocha cha maduka akitumia teknologia katika simu yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.
Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikendelea lakini waliwachwa na mshangao mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na kuwawacha wawili hao barabarani bila nguo.
Kulingana na gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na yeye hakubakia nyuma.
Mumuwe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.

NDANI YA KLABU YA YANGA, YADAIWA ZAIDI YA BILIONI MBILI ZAPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KIESCROW

Taarifa  zinadai ya kwamba zaidi ya shilingi bilioni mbili za klabu ya YANGA zimetafunwa na wajanja wasiojulikana mpaka sasa,
Inasemekana ubadhirifu huo umefanyika na baadhi ya wafanyakazi waliomaliza muda wao hivi karibuni,
Baadhi ya majina ya wafanyakazi wa zamani wakiongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo bwana Beno Njovu jana walipelekwa kituo cha polisi cha Central kuhojiwa kutokana na ubadhirifu huo.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu hiyo kimesema zaidi ya bilioni mbili zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

UNIC YAELIMISHA SIKU YA CHOO KWA VIJANA WALIO NJE YA SHULE

Siku ya choo duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 Novemba. UNIC waliadhimisha siku hii kwa kuwakutanisha vijana walioko nje ya shule tarehe 23 Desemba 2014 kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha utumiaji wa vyoo ili na wao waweze kuelimisha jamii zinazowazunguka juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo.
Tukio hili liliwakutanisha vijana toka vikundi 5: Azimio Youth Group, Makangarawe Youth Development Fund, Mashine Ya Maji Youth Development Centre,Temneke Youth Development Foundation na Tanzania Youth Development Society. Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha.
TOILET DAY 2014 3 blog 1
Vijana wakiwa katika makundi kujadili na kuweka mikakati watakavyosaidia jamii kuhusu utumiaji wa vyoo na usafi wa mazingira.
TOILOET DAY 2014 4 blog 1
Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma-Ledama akitoa mada kuhusu siku ya Choo duniani pamoja na umuhimu wa utumiaji vyoo, na kampeni maalumu ya uhamasishaji wa kuwa na vyoo.
TOILET DAY 2014 8 blog 2
TOILET DAY 2014 14 blog 2
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Vijana Temeke (Temeke Youth Development Network -TEYODEN), Ismail Mnikite akitambulisha vijana waliohudhuria kutoka makundi mbalimbali.
TOILET DAY 2014 13 blog 2
Baada ya majadiliano, vijana wakiwasilisha maazimio na mikakati waliyoyakusudia kufanya ndani ya vikundi vyao katika jamii zinazowaunguka.
TOILET DAY 2014 25 blog 2
TOILET DAY 2014 19 blog 1

Katibu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi asimamishwa kazi



        
                                            Ndg. Eliakim Maswi


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”

Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.

Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.