chini Wakati mambo yakiwa hayamuendei sawa kwenye klabu yake ya Tottenham Hotspur, mshambuliaji wa Kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor ametoa kali ya wiki kwa habari ambayo imetengeneza vichwa vya habari vingi katika ulimwengu wa michezo duniani.

Adebayor alitofautiana na mama yake na
kumfukuza mama huyo katika moja ya nyumba zake huko Togo na dada zake
wamekaririwa wakisema kwamba mchezaji huyo hapokei simu zao.
Mtandao wa allsports.com
wa Ghana umechapisha habari yenye kauli ya mmoja wa dada wa mchezaji
huyo ambaye alisema; “Kwa hivi sasa mama yetu anauza mifuko, makufuri na
vitu vingine katika mpaka wa Ghana na Togo.
Mama yetu hajamuona Adebayor kwa zaidi
ya mwaka mmoja sasa na kaka amekuwa hapokei simu anapopigiwa na mama,
mama hampigii simu ili kumuomba fedha, anataka tu kuongea na mwanae kwa
sababu anampenda sana..”

No comments:
Post a Comment