CHONDE CHONDE ULEVI NOMAA, MJESHI AZIMA KWA POMBE
Wananchi Iringa wakimtazama askari wa jeshi ambae jina halikuweza kufahamika aliyekuwa amezima kwa ulevi uliopindukia |
mjeshi huyo akiwa akiwa amezima |
Mjeshi akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita kiasi
..........................................................................................................
KATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga
Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za
jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika
mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo
mikoani mjini Iringa
Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2
usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka
katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja
mjini Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo
kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya
wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa
askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati
wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa
kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi
hilo.
Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi
ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika
kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na
kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .
Alisema
kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu
yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru
kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana
akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza
"
Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika
sare .....sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala
polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema
kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja
Maamuzi
hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na
kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana mambi ambayo
aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo
la Kihesa .
Ushauri wetu kwa askari wetu
kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa
pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa
afya yako ama chonde chonde ulevi nomaaa
No comments:
Post a Comment