Friday, November 21, 2014

Hekaheka ya Novemba 21, ni mwendelezo wa ile ya jana inayohusu mtoto kufariki kituo cha Polisi.


chini
for_the_love_ones___by_evil1302-d2z98zc
Hekaheka ya leo ni mwendelezo wa ile ya jana inayohusu mtoto wa miezi 6, aliyefariki kituo cha Polisi baada ya mama yake kushikiliwa na Polisi baada ya kufunguliwa mashtaka ya kufanya vurugu nyumbani kwa Kijumbe anayechangisha hela ya mchezo wa Upatu.
Bibi wa Mtoto huyo amesimulia kilichotokea siku ya tukio ambapo amesema alienda kituo cha Polisi kuomba apewe mjukuu wake ambaye alikuwa anaumwa Malaria ili akampatie dawa lakini wahusika aliowakuta kituo cha Polisi waligoma na kumtaka alete dawa hizo amnyweshe hapo hapo kituoni.
Mama wa mtoto huyo amesema mtoto wake alizidiwa na homa wakati wa usiku lakini Mgambo aliyekuwa zamu akagoma kumsaidia chochote, ilipofika asubuhi alikuta mtoto wake ameishiwa nguvu kabisa, baada ya mgambo kugundua kwamba amefariki  ndipo walipomruhusu arudi naye nyumbani huku mama wa mtoto akiwa hajui chochote kama mtoto wake amefariki.
Baada ya kumpokea mtoto huyo kutoka kwa mama yake aliyekuwa amembeba bibi wa mtoto huyo ndiye alikuwa wa kwanza kugundua hilo na kuwataarifu baba na majirani juu ya kifo hicho.
Leo Tena imemtafuta Kamanda Kova ambaye amesema ana taarifa juu ya tukio hilo na kuahidi kulitolea taarifa rasmi baadaye.
Kuisikiliza Hekaheka hiyo bonyeza play hapa chini.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia

No comments:

Post a Comment