Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
Afisa anayedaiwa kupangiwa
njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini
katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi
januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane
ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa maujaji.
Emir Sanusi alikuwa gavana wa benki kuu yaNigeria kabla ya kuteuliwa kama Emir Kaskazini mwa Nigeria
Emir
wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau
wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha
na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu
wa Boko Haram.
Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi. Emir
huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua
wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano
wa maombi. Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii
sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya
kisiasa.
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa
Wapiganaji wa wa Boko Haram
wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa
za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko
wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu. Sanusi
alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya
benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba
wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi
hilo. Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la
Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka
watu kujihami dhidi ya Boko Haram. Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa
wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara
kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku
wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria
kali ya kiisilamu. Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali
alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi
kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda
kutokana na mashambulizi ya kundi hilo. Mwandishi wa BBC anasema
ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee
kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram. Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment