U Heard Novemba 26 iko hapa, inamhusu msanii Linex. Unaweza kuisikiliza

Gossip Cop ameongea na Linex ambaye amesimulia namna ambavyo msanii Steve Nyerere alimkutanisha na Nyamihela
kwa ajili ya kumuuzia gari, ambapo Linex amesema magari ambayo alipewa
na jamaa huyo hayakuwa yanaendana na kiwango cha pesa alichokitoa hivyo
akamtaka amtafutie gari nyingine ambapo hakumpatia gari wala kumrudishia
pesa milioni kumi aliyompatia.
Nyamihela amesema kuwa alimpatia gari Linex
huku akiwa hajamalizia malipo ya pesa ambayo walikubaliana na baadaye
aliamua kuchukua gari lake na kumrudishia pesa shilingi milioni moja na
kiasi kilichobakia anasema ni milioni mbili tu na sio milioni kumi kama
ambavyo msanii huyo anadai.
Mahusiano yao mbali na biashara hiyo Nyamihela amesema aliwahi kumsaidia mara kadhaa Linex kwenye shughuli zake za muziki.
Nimekuwekea hapa sauti niliyoirekodi kwenye U Heard, unaweza kuisikiliza hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia facebook
No comments:
Post a Comment