chin

Arusha. Serikali imeuza kwa mnada aina
mbalimbali ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni
yaliyokamatwa wakati yakitoroshwa nje ya nchi.
Mnada huo uliendeshwa jana na mwenyekiti wa bodi
ya ushauri wa madini, Richard Kasesela akisaidiana na maofisa wa Wakala
wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), wakati wa maonyesho ya kimataifa ya madini
yanayoendelea jijini Arusha.
Meneja uthamini wa madini kutoka TMAA, George
Kaseza alisema madini yaliyopigwa mnada yalikamatwa kwenye vituo
mbalimbali vya ukaguzi, vikiwamo viwanja vya ndege na maeneo ya
mipakani.
“Madini haya yalikamatwa yakisafirishwa bila
vibali maalumu vinavyoruhusu yakauzwe nje ya nchi wala kulipiwa ushuru
na kodi ya Serikali,” alisema Kasesela.
Alisema Serikali imefikia hatua ya kupiga mnada
madini hayo baada ya kuyataifisha kutokana na amri ya mahakama baada ya
watuhumiwa waliokamatwa wakisafirisha nje ya nchi kutiwa hatiani na
baadhi kuhukumiwa vifungo au faini.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Ngozi Mwihava alisema miongoni mwa madini maarufu yaliyopigwa mnada ni
dhahabu kilo moja na tanzanite ambayo hakutaja kiasi chake.
Serikali kuanza kukamata madini yanayosafirishwa
nje ya nchi kimagendo imekuja baada ya kuweka ofisi za udhibiti wa
madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya Kilimanjaro, Mwanza na Dar
es Salaam.
Kutoroshwa kwa madini hayo kwa njia mbalimbali, kumeifanya Kenya na India kuongoza duniani kwa kuuza madini ya tanzanite.
No comments:
Post a Comment