chin

Tasnia ya muziki wa injili leo imempoteza mwimbaji wake nyota na mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo
November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, marehemu
George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es
salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda
mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.
Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji kupitia
kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the
corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi
huku akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa
Lulu. Ni takribani miaka mitatu sasa toka aliyekuwa mwalimu mkuu wa
kwaya ya Lulu kufariki dunia, kifo ambacho wengi walidhani aliyefariki
ni George kiasi kwamba taarifa za kifo chake hii leo kimepokelewa kwa
tofauti hasa baadhi ya watu wakidhani alishafariki siku nyingi.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/11/tanzia-mwimbaji-nyota-wa-injili.html#sthash.XZZiHDm5.dpufTasnia ya muziki wa injili leo imempoteza mwimbaji wake nyota na mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo
November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, marehemu
George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es
salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda
mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.
No comments:
Post a Comment