Msaada wa kumsaidia Bi Mwanaid Vuai Saleh. aliyeunguwa kwa Maji ya Moto.
Kumradhini kwa kuweka picha hii ya Bi Mwanaid Vuai Saleh, kwa maadali ya habari haifai.
Aliyepata
ajali hiyo ya kuanguka wakati akiwa katika kazi zake za nyumbani na
kuanguka katika sufuria la maji ya moto baada ya kuona kizunguzungu na
kuangukia humo na kumuathiri kiasi hicho na kwa sasa amelazwa katika
Hospitali ya Jeshi Bububu akipata matibabu ya majaraha hayo.
Bi Mwanaid Vuai ni Mkaaza wa Shehia ya Chumbuni Wilaya ya Mjini Unguja
Anaomba msaada wa Fedha ili kusafirishwa nje ya Nchi kupelekwa India kwav matibabu zaidi
Kwa
kila Mwananchi atakayepata fursa ya kumsaidi Bi Mwanaid Vuai, ili kupata
matibabu, anaombwa kuwasiliana na Mdau wa Blog hii, kwa Namba
0777424152.
Bi Mwanaid Vuai Saleh akiwa ameathirika kiasi hicho kama
anavyoonekanav pichani akiwa katika hospitali ya Jeshi Bububu Unguja
akiendelea na Matibabu yake akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili
kupata kusafirishwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi ili kurudisha hali
yake kiafya.
Kwa sasa amepata baraka zote kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kupata missada kama inavyosomeka hapo chini.
No comments:
Post a Comment