Bw Nicholas Chege Mwangi, dereva wa basi nambari KBT 903R la Githurai 44, akiwa kortini Novemba 28, 2014. Picha/PAUL WAWERU
SERIKALI
imesimamisha leseni ya kampuni ya matatu ya Nazigi Sacco kwa muda wa
wiki mbili, baada ya wahudumu wake kushtakiwa kwa kumvua mwanamke nguo
katika Barabara ya Thika.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi (NTSA) Francis Meja aliipa kampuni
hiyo wiki mbili kuwasilisha magari yao yote 243 kwa ukaguzi. Sacco hiyo
ina magari takriban 243.
Kamanda
wa Trafiki Charlton Mureithi pia atahakikisha kuwa hakuna gari lolote
la kampuni hiyo ambalo litahudumu hadi suala hilo litatuliwe.
Dereva
na makanga wa basi moja la sacco hiyo ambapo abiria mmoja mwanamke
alivuliwa nguo na kudhulumiwa kimapenzi kwa saa kadha wataendelea
kuzuiliwa kwa siku 21 zijazo, huku polisi wakiendelea na uchunguzi wao.
Bw
Nicholas Chege Mwangi na Bw Meshack Mburu Mwangi, ambao ni dereva na
utingo wa basi hilo, lenye nambari za usajili KBT 903R wanazuiliwa
katika kituo cha polisi cha Kasarani na wanatarajiwa kuwafichua
wahusika, ambao wanasemekana kutoroka.
Mahakama
Nairobi iliambiwa kuwa polisi walikuwa wakichunguza visa mbalimbali vya
dhuluma za kimapenzi, na wameanzisha uchunguzi dhidi ya visa kadha vya
dhuluma za kimapenzi na kuvuliwa nguo kwa wanawake jijini Nairobi, ili
kuwakamata na kuwashtaki wahusika.
Upande
wa mashtaka pia uliwaomba waathiriwa wa dhuluma hizo, ambao
hawajajitokeza baada ya kushambuliwa katika maeneo hayo mawili
kujitokeza ili kuandikisha taarifa kwani washukiwa hao tayari
washakamatwa.
Kuzua hofu
“Kumekuwa
na ongezeko la kuvuliwa nguo kwa wanawake pamoja na dhuluma za
kimapenzi, hali ambayo imezua hofu miongoni mwa umma. Uchunguzi
tuliofanya ulipelekea kukamatwa kwa washukiuwa mnamo Novemba 27 katika
Barabara ya Thika,” akasema Duncan Ondimu, ambaye ni kiongozi wa
mashtaka katika wasilisho lake kwa mahakama.
Katika
kesi tofauti, polisi mmoja wa utawala na abiria mmoja wa kiume
wamefikishwa mahakamani kwa kujaribu kumvua nguo msichana mmoja, aliye
mwanafunzi mmoja wa shule katika basi moja.
Watu
watano pia wameshtakiwa kwa kuwatoa wanawake nguo katika mtaa wa
Kayole. Kisa hicho, ambacho kilifanyika katika mtaa wa Kayole kingali
kinachunguzwa. Tukio la barabara ya Tom Mboya pia lingali kinachunguzwa.
Jana,
upande wa mashtaka ulisema kuwa waliwahoji washukiwa hao wawili lakini
“hawakuwa bado wamewafichua washukiwa waliohusika katika kitendo hicho”
lakini walikuwa wakifuata habari muhimu zitakazopelekea kukamatwa kwao.
Kiongozi huyo wa mashtaka alisema kuwa mhusika katika kisa cha basi la Githurai 44 bado hajatambuliwa
You might also like:
No comments:
Post a Comment