
Show kubwa ya burudani Tz ya XXL inayorushwa na Clouds FM huwa anasikika mzee wa kutoboa kila siku, Soudy Brown a.k.a Gossip Cop akitoboa story za mastaa mbalimbali.
Leo kwenye U Heard Gossip Cop katoboa kuhusu mgogoro ambao imesemekana upo kati ya mastaa wawili Irene Uwoya na Msami.
Story iliyopo ni kwamba wawili hao walipishana na katika video iliyozagaa mitandaoni inasikika sauti ya Irene akimlazimisha Msami kumpiga kibao.
Katika sauti inayosikika kwenye video hiyo majibizano yao yako hivi;
Msami : “… Si unataka nikupige.. nakupiga …”
Irene : “… Nipige saa hizi.. nataka unipige saa hizi… Nipige…”
Msami : “… Tuingie kwenye gari .. ndani tutaenda kupigana..”
Irene : “… Sitaki.. Nataka unipige kwanza.. Nipigie kibao ..Nipige, naondoka.. haya nipige…”
Msami : “…Haya nakupiga …”
Irene : “… Nguvu…”
Baada ya kupigiwa simu, Msami amekanusha kuwepo kwa ugomvi kati yao.
No comments:
Post a Comment