Kocha Alex Ferguson wa Man U amefanya mahojiano na gazeti moja huko Uingereza
(Football Focus)
na kuzungumzia mambo mengi kuhusu ufundishaji na menejiment ya timu ya
mpira wa miguu hasa wakati wake akiwa na Klabu ya Man U. Amezungumzia
mambo kadhaa ya msingi katika maeneo yafuatayo:
1. KUHUSU MAN CITY: Anasema ni timu hatari na wapinzani wao haswa kwa
sasa kama ilivyokuwa zamani ilivyokuwa Chelsea.
2. KUHUSU RVP: Sir Alex anasema hakuwahi kudhani siku moja angeliweza
kumsajili Robin Van Persie. Anasema alizungumza muda mrefu na Wenger na
majadiliano yao yalikuwa mazuri ingawa hakudhani Arsenal wangekubali
kumuuzia mchezaji huyo. Ila aligundua baadaye Arsenal waligundua RVP
anataka kuhama na hivyo ikawa rahisi kumpata.
3.UCHEZAJI WA RVP: Ni mchezaji mwenye ujuzi wa mchezo na uwezo wake
umetoa faraja kwa watu wote hapa Man U.
4. UMUHIMU WA KUHUDHURIA MAZOEZI: Sir Alex anasema hajawahi kuacha
kuhudhuria vipindi vya mazoezi hata siku moja. Uangalizi wake ni muhimu
sana katika kipindi hiki cha maisha yake.
5. SUALA LA UFUASI KATIKA MCHEZO WA MPIRA:Sir Alex anasema hivi: "Wapo
watu miongoni mwa wasaidizi/wafanyakazi wangu ambao wamekuwa na mimi kwa
miaka 20 au zaidi. Hii inaleta hali ya ufuasi kwangu na mimi kwao pia".
6.KISASILI/MYTHIOLOGIA ZAKE: Sir Alex anazungumziaje kuhusu visasili juu
ya maisha yake? "Visasili ni vingi sana juu ya maisha ya watu
waliofanikiwa. Mojawapo ya uzushi mkubwa juu ya maisha yangu ni eti
nimewahi kufanya kazi kwenye bandari. Anasema hajawahi kufanya kazi
bandarini kamwe, ila baba yake, kaka zake na wajomba zake walifanya kazi
bandarini.Sir Alex anadai kuwa alikuwa mwerevu zaidi (intelligent)
kutokufanya kazi za bandari.
7. JOSE MOURINHO: Sir Alex anadai huyu ni mtu anayependa kucheza na
mchezo wa kupandisha presha "mind game" dhidi ya timu pinzani. Huwezi
kujua atafanya nini huwa hashindani naye kwani huwezi kumshinda. Anasema
"huwa sishindani naye na huwa ananiletea chupa ya wine kila mara.
8. REAL MADRID: Nawaangali Real Madrid kila weekend usiku; aliwaangalia
wakicheza na Granada na anaamini Ronaldo alifunga goli zuri sana ila tu
ilikuwa ni siku ya Granada. Kuhusu mchezo wa Champions ligi dhidi ya
Madrid (13/2/2013) anasema anawajua uimara wao na ni lazima apange
kikosi sahihi siku hiyo ili washinde. Utakuwa mchezo mgumu sana na hawa
jamaa hawafungiki kirahisi Bernabeu.
9. WACHEZAJI KUWA MAKOCHA: Sir Alex anasema: "Tunaona hali ambapo mtu
anakuwa mchezaji leo alafu baadaye kocha.Hebu niambieni hii
inawezekanaje? Ninajisomea sana kuhusu kuwaharakisha wachezaji kuwa
mameneja eti kwasababu tu wamewahi kuwa wachezaji wa
kimataifa.Haijalishi mtu umekuwa mchezaji wa kimataifa au hujawahi
kucheza ligi yoyote, ili kuwa na mafanikio katika kazi ya umeneja wa
timu ni lazima uwe na kipindi kirefu cha kujifunza chini ya uangalizi wa
meneja mzoefu.
10.KUSTAAFU KAZI YA UMENEJA: "Hili swali linajirudia mara nyingi kadri
ninavyoendelea kuzeeka.Nadhani jambo la msingi ni kwa vipi ninajisikia.
Kadri mtu unavyozeeka hali afya haitabiriki hasa katika umri wa miaka 70
na kuendelea. Hadi sasa hivi hali yangu ya afya ni murua; ila huwezi
kujua".
No comments:
Post a Comment