Watu 6 Wafariki Dunia Usiku Wa Kuamkia Leo baada ya Magari Manne Kugongana Huko Nzega.....Hapa kuna Picha 10 Toka Eneo la Ajali
Sunday, March 22, 2015
Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi inayomkabili Chris Brown!!

Baada ya kutumikia kifungo cha miaka sita akihukumiwa kwa kosa la kumpiga aliyekuwa girlfriend wake Rihanna, kuna maamuzi ambayo mahakama ya Los Angeles imetoa kuhusiana na hitmaker wa nyimbo ya ‘New flame‘ Chris Brown.
Ni miaka sita tangu mwanamuzi Rihanna
amshtaki Chris Brown kwa kosa la kumpiga na kutumikia adhabu hiyo ambayo
alikuwa katika kipindi cha majaribio na sasa yuko huru baada ya kesi
yake kumalizika.
Katika kuonyesha furaha yake Chris Brown
baada ya kutoka mahakamani hapo aliandika kwenye ukurasa wake wa
Twitter kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa yupo huru.
“IM OFF PROBATION!!!!!!!! Thank the Lord!!!!!!”
Zitto ajiunga rasmi na Chama cha ACT-Tanzania, akabidhiwa kadi namba 007194
Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT.
...Kumwaga ‘mboga’ mbele ya wandishi wa Habari Jumapili hii Machi 22
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Hayawi
hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya
kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa
Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama
hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hii
inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika
barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi
kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza
kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.
Endelea kufuatilia EDDY BLOG kwa tukio hilo tutakalowaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo, kujua ni wapi na muda gani endelea kuperuzi nasi.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
Mwanachama rasmi wa ACT Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.
“He..he
he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi
hiyo kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi
za chama cha ACT tawi la Tegeta,
Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya kupokea kadi hiyo.
Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.
Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho mapema JANA.
Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa.
Saturday, March 21, 2015
NEWS ALERT: NYUMBA ILIYOPO NDANI YA MSIKITI SOWETO YATEKETEA YOTE KWA MOTO MAPEMA LEO.
Jengo
lililopo ndani ya Msikiti wa Soweto Limeteketea kwa moto Mapema leo
chanzo hakijafahamika bado Moto huo umeteketeza nyumba yote, japo kuwa
wananchi na waumini walijitahidi kuzima lakini ulionekana ni mkubwa
sana, Hata hivyo wananchi wamelaumu Kikosi cha zimamoto kwa kuwa
walipewa taarifa mapema lakini hawakuweza kufika kwa muda katika eneo
hilo. Endelea kufuatilia tukio hili hapa kwa taarifa zaidi.
No comments:
Post a Comment