Shambulio la Balozi wa MAREKANI Korea Kusini

Balozi huyo alikimbizwa Hospitali ambako
alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili kwenye jeraha na pia
ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa, huku baadhi ya mishipa
ikishindwa kufanya kazi ingawa madaktari wamesema hakuna athari yoyote
itakayotokana na majeraha hayo.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa Polisi walifanikiwa kumkamata Kim Ki-Jong akihusishwa na tukio hilo huku kukiwa na taarifa za jamaa huyo kufanya kosa kama hilo mwaka 2010 alipomshambulia Balozi wa Japan nchini Seoul.
Rais wa Marekani Barack Obama amempa pole Balozi huyo.
Msemaji wa baraza la maridhiano na
ushirikiano ambaye ndiye muandaaji wa mkutano huo ameomba radhi kwa
kutokuwa na ulinzi mzuri uliosababisha Balozi huyo kushambuliwa.



No comments:
Post a Comment