Wednesday, March 11, 2015


Shilole Aendeleza Vipigo Kwa Nuh

Shilole Aendeleza Vipigo Kwa Nuh
Mwanadada Staa wa Bongo Movie na Bongo Fleva , Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, ameendeleza tabia yake ya kumpa vipigo vya mara kwa mara mpenzi wake, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye pia ni msanii.
Habari kutoka vyanzo vya kuaminika vinasema Shilole alimdunda kwa mara nyingine Nuh wiki iliyopita, baada ya kutokea kutoelewana baina yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
“Ninampenda sana mume wangu na ninamheshimu, hili suala linapozungumzwa au kuulizwa linaniumiza sana, haya ni mambo ya muda mrefu na yameshamalizika,” alisema msanii huyu ambae ni mama wa watoto wawili.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa, simu yake haikupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu jambo hilo pia hakujibu. Lakini kwenye ukurasa wake mtandaoni aliandika “Baby we nipige tu ila usiniumize tu sura yangu ….mapenzi bila wivu hayaendi” na kuweka picha akiwa na Shilole.
Hii siyo mara ya kwanza kwa wapenzi hao kukwaruzana, kwani imeshawahi kutokea siku za nyuma hadi kufikia wakati wakatengana.

No comments:

Post a Comment